Maghala mawili ya
kuhifadhia nyuzi yaliyopo katika kiwanda cha nyuzi mjini Tabora kinachomilikiwa
na mwekezaji mwenya asili ya kiasia, yameteketea kwa moto tangu saa 7 mchana na
kusababisha hasara kubwa ambayo haikujulikana mara moja.
Mkuu wa kikosi cha zimamoto manispaa ya Tabora Bw. Farijara
ameiambia ITV katika harakati za kuzima moto huo usisababishe madhara sehemu ya
uzalishaji, moto huo haukuleta madhara kwa binadamu na chanzo bado
hakijajulikana.
Mmiliki wa kiwanda hicho amesema kuwa hasara iliyojitokeza
katika sehemu hiyo ni kubwa, lakini haitaathiri sehemu ya uzalishaji kutokana
kuwa na malighafi sehemu nyingineambazo hazijateketea kwani sehemu iliyoteketea
ni sehemu ya mali ambayo ilikuwa imesindikwa tayari.
Hata hivyo watumishi wa kiwanda hicho wamemshukuru Mungu
kutokana na moto huo kuwaka wao wakiwa mapumziko ya chakula, kwani ingeweza
kuleta madhara kwa maisha ya watu ambao hufanya kazi ndani ya maghala
hayo, huku wakisikitikia hasara iliyojitokeza
kwani ni sehemu ya uzalishaji wa kiwandani hapo.
Nahizo zilikuwa na halakati za kuokoa baathi ya vitu wakati moto ukuendelea kushika kasi katika jengo hilo.
0 maoni:
Chapisha Maoni