PAMBANO
LA YANGA, MGAMBO SHOOTING LAINGIZA MIL 37/-
SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANA ALHAMISI

RAIS
WA CAF AMPONGEZA MALINZI
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal
Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Katika
salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu
Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya
kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.
Amesema
CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira wa miguu
havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla, na kuongeza
kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha zaidi vijana wa bara hili.
Rais
Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha uongozi
na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele gurudumu la
kuendeleza mpira wa miguu.
PAMBANO
LA YANGA, MGAMBO SHOOTING LAINGIZA MIL 37/-
Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting lililochezwa jana
(Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 37,915,000.
Washabiki
waliohudhuria mechi hiyo namba 46 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa
mabao 3-0 walikuwa 6,515 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh.
15,000 na sh. 20,000.
Mgawo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
5,783,644.07, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,145,790 wakati kila klabu ilipata
sh. 8,550,741.95.
Wamiliki
wa uwanja walipata sh. 4,347,834.89, gharama za mchezo sh. 2,608,700.93, Bodi
ya Ligi sh. 2,608,700.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,304,350.47, Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
1,014,494.81.
SIMBA,
KAGERA SUGAR KUUMANA KESHO
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi
kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuanzia saa 10 kamili jioni.
Viingilio
katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1
vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.
Nayo
Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi
hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Novemba
2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya),
Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino
Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi
hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa
mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka
huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera
Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs
Mtibwa Sugar.
Novemba
7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni