England hatarini kuzivaa Hispania, Ujerumani
ENGLAND ipo kwenye hatari ya kupangwa na Brazil, Hispania au
Ujerumani kwenye hatua ya 16 bora kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwakani iwapo haitaongoza kundi lao kwenye fainali hizo.
Habari hizo zimewashtua baada ya jana Jumatano kubainika kwamba England inayonolewa na Roy Hodgson haitakuwa kwenye orodha ya timu nane vigogo ambavyo vitapewa hadhi ya kuongoza makundi ya michuano hiyo.
Licha ya kuwapo kwenye 10 bora ya viwango vya ubora wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) vinavyotarajia kutolewa leo Alhamisi baada ya ushindi mfululizo dhidi ya Montenegro na Poland, hilo bado halitoshi kuwafanya kuwamo kwenye orodha ya timu zenye hadhi ya kubeba makundi.
Jambo hilo linaifanya England kupambana kuhakikisha inaongoza kundi lake itakalopangiwa ili kujiondoa kwenye nafasi ya kumenyana na vigogo hivyo katika hatua hiyo.
Mapema mwezi huu, Fifa ilitangaza Brazil itakuwa timu ya kwanza itakayobeba kundi, wakati timu nyingine zinazopewa nafasi zikiwa Hispania, Argentina, Ujerumani, Ubelgiji na Italia.

0 maoni:
Chapisha Maoni