Ijumaa, 15 Aprili 2016

Korea Kaskazini yashindwa katika kurusha kombora


KimImage copyrightAP
Image captionImekuwa siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Il-sung
Korea Kaskazini imefanya jaribio la kufyatua kombora katika pwani yake ya mashariki, lakini dalili zinaonesha jaribio hilo halikufanikiwa, maafisa wa Marekani na Korea Kusini wanasema.
Bado haijabainika roketi iliyotumiwa ilikuwa ya aina gani lakini inadhaniwa majaribio hayo yalikuwa ya kombora la masafa la wastani kwa jina “Musudan” ambalo taifa hilo lilikuwa halijalifanyia majaribio.
Shughuli hiyo ilikuwa ikifanyika siku ambayo ni ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Il-sung.
Imetokea huku hali ya wasiwasi ikiwa imetanda rasi ya Korea.
Shirika la habari la Korea Kusini Yonhap, likinukuu duru za serikali, limesema kombora hilo lilikuwa aina ya kombora la Musudan, ambalo kitaalamu hujulikana kama BM-25.
Majuzi, wanajeshi wa Korea Kaskazini walionekana wakisafirisha makombora mawili ya aina hiyo.
Shirika hilo limesema habari hizo zikithibitishwa, basi itakuwa mara ya kwanza kwa Korea Kaskazini kufanyia majaribio makombora ya Musudan, na huenda ikawa na makombora 50 zaidi.
Jina Musudan linatokana na kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Korea Kaskazini ambapo kituo cha kurushia makombora hayo kimejengwa.
Makombora hayo yanaweza kufika umbali wa kilomita 3,000 na kufikia kambi ya majeshi ya Marekani iliyopo kisiwa cha Guam katika bahari ya Pasifiki. Hata hivyo hayawezi kufika Marekani bara.
KimImage copyrightReuters
Image captionRais Kim Jong Un amekuwa akitishia Korea Kusini na Marekani
Marekani imesema imekuwa ikifuatilia jaribio hilo la kurusha kombora, lakini bado haijaweza kuthibitisha habari zaidi.
Korea Kaskazini, chini ya kiongozi wake wa sasa Kim Jong-un, imekuwa ikitishia kushambulia Marekani na Korea Kaskazini tangu kuwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa kwa kufanya jaribio la nne la makombora ya nyuklia.
Siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Korea Kaskazini, babu yake Kim, huwa muhimu sana kwa taifa hilo. Miaka minne iliyopita, Korea Kaskazini ilijaribu kusherehekea kwa kuzindua kombora lakini juhudi hizo zikafeli.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Korea Kaskazini yashindwa katika kurusha kombora Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top