Jumanne, 15 Machi 2016

Shabiki asubiria mkeka wa milioni 150 kama Leicester ikiwa bingwa.

Shabiki anayejiamini kupita kiasi amepiga chini dili la watu ambao wanataka kununua bet ticket yake kwa gharama ya Pound 25,000. Baada ya ushindi wa jana amepata sababu ya ziada ya kujiamini zaidi akisubilia ligi iishe ambapo anaweza kushinda Pound 50,000.
Shabiki huyu ni mmoja kati ya mashabiki watatu ambao wali bet kwa 5000/1 kwamba Leicester itachukua ubingwa msimu huu. Betting hiyo ilifanyika mwanzoni kabisa mwa msimu huu.
Mmoja kati ya mashabiki hao watatu amekubali kuuza mkeka wake ambapo aliweka Pound 10 na ameuza kwa Pound 25,000.
Alipoulizwa kuhusu matumizi ya pesa zake kama Leicester ikishinda ubingwa shabiki huyo amesema, “Nadhani kitu kimoja wapo nitaenda holiday na familia kutembelea Disney land na nyingine kufanya mambo mengine”
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Shabiki asubiria mkeka wa milioni 150 kama Leicester ikiwa bingwa. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top