AZAM FC imejiongezea pointi tatu katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Stand United jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee, beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Shomary Salum Kapombe kipindi cha pili baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza.
Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee, beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Shomary Salum Kapombe kipindi cha pili baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza.
Wachezaji wa Azam FC wakiwa wamemzingira Kapombe kumpongeza baada ya kuifungia timu yake bao pekee |
Kapombe alifunga bao hilo dakika ya 64, akimalizia krosi ya Nahodha John Raphael Bocco aliyeingia kutokea benchi kipindi cha pili.
Azam FC sasa inafikisha pointi 50 sawa na mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi 21, zikiwa nyuma ya vinara, Simba SC wenye pointi 54 za mechi 23.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Shomari, Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Serge Wawa, Jean Baptiste Mugiraneza, Frank Domayo, Mudathir Yahya/Kipre Balou dk79, Allan Wanga/John Bocco dk64, Kipre Tchetche na Farid Mussa/Waziri Salum dk65.
Stand United: Frank Muwenge, Nassor Said ‘Chollo’, Suleiman Mrisho, Revocatus Richard, Assouman N'guessang, Jocob Masawe, Pastory Athanas, Amri Kiemba, Frank Hamis, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Salum Kamana dk80 na Haruna Chanongo/Vitaris Mayanga dk68.
0 maoni:
Chapisha Maoni