Jumanne, 29 Machi 2016

KAZIMOTO: WADOGO ZETU HAWAAMBILIKI, WANAJIONA WAO NDIYO WAO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIUNGO mkongwe wa wa kimataifa wa Tanzania, Mwinyi Kazimoto Mwitula(pichani kushoto)anayechezea Simba SC ya Dar es Salaam amesema kwamba wachezaji chipukizi wa sasa sasa wengi hawashauriki.
Akizungumza na BANDOLA.BLOGSPORT.COM jana, Kazimoto amesema kwamba wachezaji vijana wadogo wa siku hizi ni wajuaji na mambo ya mitandao ndiyo yanawaharibu kabisa.
“Huwezi kumshauri kijana wa siku hizi akakuelekwa, kwanza ataona unamuonea wivu, na haya mambo ya mitandao tena, wakisifiwa kidogo wanajua, basi inakuwa tabu,”amesema.
Kazimoto amesema kwamba inakuwa vigumu kwao wachezaji wakongwe kuwashauri vijana hata wanapoona wanakwenda ovyo na wanaweza kujiharibia maisha yao ya soka, kwa sababu ni viburi.
Mwinyi Kazimoto (wa pili kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' kulia na Ibrahim Hajib (kushoto)

“Tumebaki kuwaangalia tu, atakayeweza kujitambua mwenyewe na kujua anakosea, atakuja kwetu wakubwa tumpe ushauri,”amesema Kazimoto. 
Kazimoto alikuwa anazungumzia nidhamu na maadili ya wachezaji nyota chipukizi kuanzia ndani na nje ya Uwanja, ambavyo kwa kiasi kikubwa haviridhishi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: KAZIMOTO: WADOGO ZETU HAWAAMBILIKI, WANAJIONA WAO NDIYO WAO Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top