Johan Cruyff akiiongoza Barca kuingia Uwanja wa Nou Camp Januari 8, mwaka 1977 kumenyana na Rayo Vallecano katika mchezo wa La Liga
BODI ya Wakurugenzi ya Barcelona itakutana Jumanne kujadili namna ya kumuenzi gwiji wake, Johan Cruyff, aliyefariki dunia wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa gazeti la michezo la kila siku Katalunya, Sport, ni kwamba dhamira ya Blaugrana ni kuubadili jina Uwanja wa Nou Camp na kuupa jina la gwiji huyo wa Uholanzi ambaye enzi za uhai wake alifanya kazi kama mchezaji na kocha.
Cruyff aliyefariki dunia Alhamisi baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani akiwa na umri wa miaka 68, ameshinda mataji ya La Liga na Copa del Rey uwanjani hapo akiwa na Barca, kabla ya kutwaa mataji mengine kibao akiwa kocha likiwemo Kombe la Ulaya mwaka 1992.
Barcelona inatafakari namna ya kumpa heshima ya kudumu Cruyff kutokana na mchango wake mkubwa kwa klabu hiyo enzi za uhai wake.
Mtoto wa kiume wa Cruyff, Jordi, ambaye kama baba yake amechezea Barca na Uholanzi, alikutana na Makamu wa Rais wa klabu, Jordi Cardoner kuanza kujadili mpangop huo Jumapili.
0 maoni:
Chapisha Maoni