Ijumaa, 26 Februari 2016

MABINGWA WATETEZI WA FA CUP MAJARIBUNI LEO

Na Baraka Mbolembole
Watakuwa ugenini Nangwanda Sijaona, Mtwara kucheza na wenyeji wao Ndanda SC. ‘Wana-Kuchele’ watakuwa nyumbani katika mchezo wa pili mfululizo wa michuano hiyo, awali waliifunga Mshikamano FC magoli 5-0 katika mchezo wa raundi ya timu 32 bora. Straika, Atupele Green alifunga ‘Hat-trick’ katika mchezo huo na ndiye kinara wa magoli hddi sasa.Mabingwa watetezi wa kombe la Shirikisho (FA Cup) timu ya JKT Ruvu ya Pwani leo Ijumaa watakuwa na mtihani mkubwa kuhakikisha wanatinga hatua ya robo fainali na kuendelea kutetea ubingwa wao waliotwaa mwaka 2002 (mwaka wa mwisho yalipofanyika mashindano hayo kabla ya kurejeshwa msimu huu.)
JKT Ruvu chini ya mwalimu mzoefu, Abdallah ‘King’ Kibadeni ilifanikiwa kuwatoa Lipuli FC ya Iringa katika mzunguko uliopita kwa ushindi mwembamba wa goli 1-0 katika uwanja wa Samora, Iringa.
“Tumekuja Mtwara tukijua kwamba tumekuja kupambana na wenyeji wagumu, lakini tutapambana ili kuingia robo fainali. Sisi tunajua kwamba Ndanda ni timu nzuri, lakini pia imepewa faida ya kucheza nyumbani mechi ya pili mfululizo na sisi itakuwa mechi ya pili mfululizo tunacheza ugenini.”
“Ni kama wametengenezewa mazingira mazuri ya kupita lakini sisi tumekuja tukijua yote hayo, tutapambana ili tuondoke na ushindi.” anasemba katibu mkuu wa JKT Ruvu, Ramadhani Madeeka.
Timu hizo mbili zilikutana Nangwanda katika mchezo wao wa mwisho baina yao na wenyeji walilazwa 1-0 katika mchezo huo wa ligi kuu.
“Tumejiandaa vizuri na tumejiandaa ili kupata ushindi, kakini tunajua JKT Ruvu ni timu nzui na walitufunga mechi iliyopita hapa. Kuhusu kucheza mfululizo nyumbani naweza kusema sisi tunafuata ratiba inayopangwa, waje wacheze mpira na aliyejiandaa kwa ushindi auapata ushindi”, anasema Selemani Kachele katibu mkuu wa Ndanda SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: MABINGWA WATETEZI WA FA CUP MAJARIBUNI LEO Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top