Jumatano, 17 Februari 2016

Jumla ya wajumbe kumi na tatu wa kamati ya Siasa ya wilaya ya Singida mjini wa chama cha mapinduzi CCM wametakiwa kuondolewa katika kamati ya siasa ya wilaya hiyo



Kaimu katibu wa ccm wialaya ya Singida mjini bw,Elineema Nasari  amesema mapandekezo ya kuondolewa yamefikiwa jana katika kikao cha kutathimini uchaguzi mkuu
Amesema katika tahtimini hiyo wajumbe hao kumi na tatu wameonekana kukihujumu chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kuanzia katika kura za maoni.
Aidha Bw, amesema kamati ya siasa ya wialaya inajumla ya wajumbe kumi na saba ambapo kati yao wajumbe wanao baki katika kamati hiyo ni wanne akiwemo Meya wa manispaa bw, Mbwae Chima, Mbunge wa jimbo la Singida mjini bw,Mussa Sima katibu wa madiwani pamojana katibu wa chma hicho wilaya.

Mapendekezo hayo yanatarajiwa kupelekwa katika kamati ya Siasa mkoa kwa ajili ya kutoa uamzi
Source:Habarileo (mashambulizi)
Ed;
Date: February 17, 2016
ARUSHA
Raia wa Nchi za Afrika Mashariki wataanza kutumia paspoti za kielektroniki ambazo zitatumika kurahisisha usafiri kwa wananchi wa eneo hilo.

Mkuu wa mawasiliano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Owora Richard Othieno amesema kuanzia mwezi Machi, raia wa nchi za Afrika Mashariki wanaweza kupata pasi za kusafiria za kielektroniki za jumuiya hiyo ya kiuchumi, ili kusahilisha usafiri katika nchi hizo.












Source:srfm (Siasa)
Ed;
Date: February 17, 2016
SINGIDA






Mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka chuo St John kilichopo mjini Dodoma Bw Lingson Kasomwa amesema uchu wa madaraka kwa baadhi ya viongozi wa bara la Africa umesababisha baadhi ya viongozi kukaa madarakani kwa kipindi kirefu huku wakiendelea kuukandamiza upinzani

Akizungumza na standard radio kwa njia ya simu kuhusu mwenendo wa kampeni za uchaguzi nchini Uganda Bw Kasomwa amesema viongozi waliopo madarakani wanatumia vyombo vya dola kuukandamiza upinzani hasa wakati wa kampeni




Amesema kitendo cha mpinzani mkuu wa Uganda Dr Kiiza Besije kukamatwa na kushikiliwa mara kwa mara wakati wa kampeni kililenga kudhoofisha nguvu ya upinzani na kutoa nafasi kwa chama tawala kuendelea kukaa madarakani
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Jumla ya wajumbe kumi na tatu wa kamati ya Siasa ya wilaya ya Singida mjini wa chama cha mapinduzi CCM wametakiwa kuondolewa katika kamati ya siasa ya wilaya hiyo Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top