Mwenyekiti wa chama cha
ACT- Wazalendo, Bi Anna Mughwira amewahimiza waandishi wa habari mkoani Singida
kutumia taaluma yao kuwaelimisha wazazi na walezi juu ya madhara watakayopata
wanafunzi watoro,ili waweze kutoa ushirikiano wa kukomesha vitendo hivyo.
Amesema vitendo vya utoro
na mimba kwa wanafunzi havivumiliki,kwa madai vinasababisha wahusika kukosa
haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Kwa hali hiyo,mwenyekiti
huyo amewataka waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele kukomesha vitendo vya
utoro mashuleni.
Aidha,ameitaka radio
standard ya mjini hapa,kuangalia uwezekano wa kuandaa kipindi maalum kwa ajili
ya kutoa elimu juu ya madhara yanayosababishwa na utoro mashuleni.
0 maoni:
Chapisha Maoni