Jumapili, 10 Januari 2016

Saudia yashambulia wagonjwa Yemen, yauwa kadhaa

Katika kuendelea na jinai zake huko Yemen, ndege za kivita za muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia zimeishambulia hospitali moja kaskazini mwa nchi hiyo.
Televisheni ya al Mayadeen ya nchini Lebanon imeripoti kuwa ndege za kivita za Saudia leo zimeipiga kwa makombora hospitali moja katika mkoa wa Sa'ada kaskazini mwa Yemen ambayo inaendeshwa na Jumuiya ya Madaktari wasio na Mipaka na kuuwa wagonjwa wasiopungua watano na kujeruhiwa wengine kumi.
Ndege za kivita za Saudi Arabia pia zimeyashambulia maeneo ya al Asdad na Marih katika mkoa wa Sa'ada na kuuwa raia kadhaa. Ndege za Saudia pia zimelishambulia soko moja katika mji wa Razih kwenye mkoa huo wa Sa'ada na kuuwa watu watatu na kujeruhi wengine watano.
Katika upande mwingine makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen yamejibu jinai za Saudi Arabia kwa kufanya operesheni katika baadhi ya maeneo ya Jizan na Najran kusini mwa Saudia na kuwatia mbaroni wanajeshi kadhaa wa Saudi Arabia.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Saudia yashambulia wagonjwa Yemen, yauwa kadhaa Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top