Wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano makubwa ya kulalamikia kukamatwa na kuendelea kushirikiwa kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Televisheni ya Press TV imeripoti kuwa, maandamano hayo yamefanyika katika mikoa mitano tofauti ya Nigeria na waandamanaji wametaka kuachiliwa huru mara moja mwanachuoni huyo bila ya masharti yoyote.
Waandamanaji hao wametaka pia kuachiliwa huru mamia ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky waliotiwa mbaroni na jeshi la Nigeria.
Mwezi uliopita, jeshi la Nigeria lilifanya mashambulizi ya kikatili dhidi ya Waislamu katika mji wa Zaria, wakaua watu wengi na wakamjeruhi vibaya kwa risasi kadhaa Sheikh Zakzaky kabla ya kumtia mbaroni na kumpeleka kusikojulikana.
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imesema kuwa, makumi ya Waislamu wanaendelea kushikiliwa na jeshi licha ya hali yao kuwa mbaya kutokana na majeraha. Aidha imesema, jeshi la Nigeria linawanyima hata matibabu majeruhi hao. Kwa uchache mmoja wa Waislamu huyo ameshafariki dunia kutokana na majeraha.
0 maoni:
Chapisha Maoni