Katika
hali isiyokuwa ya kawaida waumini wa kanisa katoliki mjini Shinyanga
wamejikuta wakipigwa bumbuazi/kushangaa baada ya kufika katika kanisa la
Mama mwenye Huruma la Ngokolo mjini Shinyanga kwa ajili ya ksuhiriki
Ibada ya Mkesha wa Pasaka,ambapo kila mmoja alilazimika kukaguliwa kama
amebeba silaha na kuingia nayo kanisani.Malunde1 blog imeshuhudia
waumini wengi wa kanisa hilo wakiwa wanakaguliwa na askari wa jeshi la
polisi usiku wa kuamkia leo huku sababu ikitajwa kuwa ni kuimarisha
usalama kwa waumini ili washerehekee sikukuu kwa amani zaidi-Picha zote
na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Muonekano wa kanisa Katoliki la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga-
Waumini
wa kanisa katoliki wakiwa nje ya kanisa la Mama Mwenye Huruma
wakisubiri kukaguliwa-Kitendo cha kukaguliwa kabla ya kuingia kanisani
kinaelezwa kuwa hakijawahi kutokea katika kanisa hilo.
Askari
akimkagua muumini.Hata hivyo akizungumza na Malunde1 blog kwa njia ya
simu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha aliwaondoa
hofu wananchi na kudai kuwa zoezi hilo ni la kawaida tu.
"Hizi
ni taratibu za kiusalama,wala hakuna haja ya mtu kuhoji,kwani hivi sana
kuna watu wanadiriki kuingia na silaha makanisani mfano huko Kisarawe
kuna mtu kakamatwa na silaha kanisani,hali ambayo inatishia usalama,kwa
hiyo zoezi hili ni la kawaida tu hakuna haja ya kushangaa,tunataka
wananchi washerehekee sikukuu kwa amani zaidi",alisema Kamanda Kamugisha
Zoezi la ukaguzi linaendelea-waumini hao walilazimika kupanga mstari ,na kuanza kukaguliwa mmoja
baada ya mwingine na kuruhusiwa kuingia kanisani jambo ambalo
liliwashanghaza kwani haijawahi kutokea ikiwa ni mara yao ya kwanza
kukaguliwa kama wana silaha.
Waumini wakisubiri kukaguliwa katika foleni ya wanawake
Kila mmoja alikaguliwa
Nje ya kanisa
Malunde1
blog inalipongeza jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kuimarisha
usalama wa wananchi na mali zao katika sikukuu hii ya Pasaka. Tuwataka
wananchi kusherehekea kwa amani sikukuu hii.Lakini pia tunataka pale
mnapotoka majumbani muache walau mtu mmoja wa kulinda nyumba kutokana na
ukweli uliopo kwamba baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kutumia fursa
za sikukuu kufanya uhalifu.
Jumapili, 5 Aprili 2015
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni