TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 16, 2015
MICHUANO YA KOMBE LA TAIFA YAINGIA RAUNDI YA PILI
Michuano
ya Kombe la Taifa kwa Wanawake inaingia raundi ya pili kesho (Januari
17 mwaka huu) kwa mechi za kwanza za raundi hiyo zitakazochezwa katika
miji ya Bukoba, Arusha, Mlandizi, Dar es Salaam na Katavi.
Jijini
Dar es Salaam kutakuwa na mechi mbili ambapo mkoa wa kisoka wa Ilala
utacheza na Mtwara kwenye Uwanja wa Karume, wakati Uwanja wa Chuo cha
Bandari uliopo Tandika utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Temeke na
Dodoma.
Mechi
nyingine za michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin zitakuwa
kati ya Kagera na Mwanza itakayochezwa mjini Bukoba, Arusha na Tanga
(Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid), Pwani na Kinondoni (Uwanja
Mabatini, Mlandizi), na Katavi na Mbeya zitakazoonesha kazi kwenye
Uwanja wa Azimio.
Nazo
Ruvuma na Iringa zitacheza Januari 19 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Majimaji. Mechi hiyo itachezwa tarehe hiyo ili kusubiri matokeo ya mechi
ya marudiano kati ya Shinyanga na Simiyu.
Kamati
ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) ilikutana jana (Januari 15 mwaka huu) kupitia ripoti ya mechi ya
marudiano ya raundi ya kwanza kati ya Shinyanga na Simiyu ambayo
ilivunjwa na mwamuzi katika daika ya 70.
Baada
ya kupitia ripoti, Kamati imebaini kuwa licha ya vurugu alizofanyiwa
mwamuzi, bado mechi hiyo ingeweza kuendelea kwa kuchezeshwa na mwamuzi
wa akiba kwa vile usalama ulikuwepo baada ya yeye kupigwa.
Pia
Kamati imeagiza Katiba wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Simiyu,
Emmanuel Sologo aliyeripotiwa kumpiga mwamuzi suala lake lipelekwe
kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi, wakati Kocha wa Simiyu,
Emmanuel Babu ambaye naye alishiriki kumpiga mwamuzi amesimamishwa
wakati akisubiri kuchukua hatua zaidi.
Kamishna wa mechi hiyo Idd Mbwana, na mwamuzi Joseph Pombe wamefungiwa kwa miaka miwili.
Mechi
kati ya Shinyanga na Simiyu itamaliziwa dakika kumi zilizobaki kesho
(Januari 17 mwaka huu) mjini Shinyanga. Kila chama cha mkoa kitabeba
gharama zake katika uendeshaji wa mechi hiyo ambayo mwenyeji ni Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA).
Timu
itakayosonga mbele baada ya mechi hiyo itacheza mechi ya kwanza ya
raundi ya pili ugenini Januari 19 mwaka huu dhidi ya Kigoma. Mechi za
marudiano za raundi ya pili zitachezwa kati ya Januari 21 na 22 mwaka
huu.
Hatua
ya robo fainali hadi fainali ambayo mechi zake zitachezewa jijini Dar
es Salaam itaanza Januari 26 mwaka huu. Fainali itachezwa Februari Mosi
mwaka huu.
Vilevile
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya TFF imemfungia kwa miaka miwili
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (SIREFA),
Gabriel Gunda kwa kushindwa kuingiza timu yake uwanjani kwenye mechi ya
marudiano ya raundi ya kwanza dhidi ya Dodoma iliyokuwa ichezwe kwenye
Uwanja wa Namfua mjini Singida.
AMAVUBI KUTUA MWANZA JANUARI 21
Timu
ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) inawasili Mwanza, Januari 21 mwaka huu kwa
ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars Maboresho
itakayochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Amavubi
yenye msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na
viongozi itawasili kwa ndege ya RwandAir na siku hiyo hiyo jioni
itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Timu hiyo itafikia kwenye
hoteli ya JB Belmont.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaingia kambini keshokutwa
(Januari 18 mwaka huu), na siku inayofuata itakwenda Mwanza tayari kwa
ajili ya mechi hiyo itakayofanyika Januari 22 mwaka huu.
Kikosi
hicho cha Kocha Mart Nooij ambacho ni sehemu ya maandalizi ya mechi za
mchujo za michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani
(CHAN) kinaundwa na wachezaji 26.
MAREKEBISHO YA MECHI ZA VIPORO VPL
Ratiba
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imeingizwa mechi za viporo zilizotokana na
timu za Azam, Mtibwa Sugar na Simba kucheza michuano ya Kombe la
Mapinduzi 2015 iliyomalizika wiki hii kisiwani Zanzibar.
Vilevile
mechi za viporo zimeingizwa kwa kuzingatia ushiriki wa timu za Azam
kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Yanga kwenye Kombe la Shirikisho
(CC) pamoja na mechi za kirafiki za Taifa Stars.
Yanga
itacheza na BDF ya Botswana kwenye mchezo utakaofanyika Februari 14
mwaka huu Uwanja wa Taifa wakati Azam itaikabili El Merreikh ya Sudan
kwenye Uwanja wa Azam Complex, Februari 15 mwaka huu.
Mechi
za viporo itakuwa kama ifuatavyo; Januari 20- Kagera Sugar na Azam
(Mwanza), Januari 28- Simba na Mbeya City (Dar es Salaam), Februari 4-
Coastal Union na Yanga (Tanga), Februari 11- Azam na Mtibwa Sugar (Dar
es Salaam) na Februari 11- Mgambo Shooting na Simba (Tanga).
Februari
11- Yanga na Ndanda (Dar es Salaam), Februari 21- Mbeya City na Yanga
(Mbeya), Februari 25- Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons (Morogoro),
Februari 28- Simba na Mtibwa Sugar (Dar es Salaam), Machi 4- Ruvu
Shooting na Azam (Pwani), na Machi 4- JKT Ruvu na Yanga (Dar es Salaam).
Machi
4- Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro (Morogoro), Machi 8- Simba na Yanga
(Dar es Salaam), Machi 11 Azam na Mbeya City (Dar es Salaam), Machi 11-
Yanga na Kagera Sugar (Dar es Salaam), Machi 18- Azam na Ndanda (Dar es
Salaam), Machi 18- Yanga na Stand United (Dar es Salaam), Aprili 8-
Simba na Tanzania Prisons (Dar es Salaam).
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Home
>
Untagged
0 maoni:
Chapisha Maoni