Jumapili, 5 Oktoba 2014

Zanzibar yahitaji kuwekeza katika walimu

Zanzibar yahitaji kuwekeza katika walimu

arehe tano mwezi Oktoba ikiwa ni Siku ya Walimu Duniani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO limesisitiza umuhimu wa mafunzo kwa walimu.
Kwa mujibu wa takwimu za UNESCO, nusu ya walimu wanaofundisha nchini Sudan Kusini, Senegal, Guinea-Bissau na Angola hawakufikia kiwango cha elimu kinachotakiwa kwa kuwa mwalimu.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesisitiza umuhimu wa kuajiri walimu wanaohitajika shuleni, lakini pia kufundisha wale ambao wameshaajiriwa.
Nchini Tanzania hali ikoje? Katika kisiwa cha Zanzibar, walimu wanakumbwa na matatizo mengi. Abdulrahman Said ni mwanahabari kutoka mtandao wa wanahabari watoto unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Ametembelea shule ya Bumbwini, Kaskazini mwa Zanzibar ili kupata maoni ya wanafunzi kuhusu jinsi ya kuboresha hali ya walimu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Zanzibar yahitaji kuwekeza katika walimu Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top