UTEKAJI WATOTO WAZIDI KUTIKISA DAR
Wanafunzi wa shule ya msingi wakitoka madarasani baada kutokea kwa hali ya vurugu.
MUNGU
wangu! Lile sakata la utekaji na upoteaji wa watoto ambao wengi ni
wanafunzi wa shule za msingi katika Jiji la Dar na kudaiwa linafanywa na
watu walio kwenye magari aina ya Toyota Noah limeingia katika sura
nyingine.
Safari hii,
gari moja lilitupiwa mawe na dereva nusura kuuawa kufuatia kufika katika
Shule za Msingi za Kombo na Mtakuja zilizopo Vingunguti, Dar kwa lengo
la kuzungumza na walimu kuhusu mikopo lakini likahofiwa lilikwenda
kuteka watoto.
Tukio
hilo lilijiri Ijumaa iliyopita na kusababisha vurugu kubwa kati ya
wazazi na walimu hali iliyowafanya maafande wa Kituo cha Polisi Buguruni
kuwasili katika eneo la tukio ili kutuliza ghasia na kwanusuru walimu.
Mmoja wa walimu akiwa na wanafunzi hao. UWAZI ENEO LA TUKIO
Gazeti hili lilifika eneo la tukio muda mfupi na kuwakuta walimu
wakiwa chini ya ulinzi wa polisi ili wasishambuliwe na wazazi ambao
walivamia shule wakidai kwamba watoto watatu walitekwa na watu wenye
Noah jeusi.
SABABU YA VURUGU
Vurugu hizo zilizoanza saa nne asubuhi siku hiyo zilitokea baada ya
gari moja jeusi aina ya Toyota Noah kufika shuleni hapo na kushambuliwa
na wananchi wakidai kwamba ndilo linalotumika kuwatekea watoto wao
shuleni hapo.
Baadhi
ya wazazi na wananchi wakiwa wametanda eneo la Shule za Kombo na
Mtakuja zilizopo Vingunguti, Dar. Mmoja wa wazazi aliyejitambulisha kwa
jina la Huma Selemani alisema Noah hilo la mikopo kwa walimu lililokuwa
na vioo vyeusi lilihisiwa ni la utekaji baada ya jana yake (Alhamisi)
ambapo gari kama hilo lilifika shuleni hapo na dereva kumuuliza mmoja wa
wanafunzi sehemu ambapo mwanafunzi huyo akasema haijui.
Ilidaiwa kuwa, pamoja na denti huyo kusema haijui sehemu hiyo
walimchukua na kumuingiza ndani ya gari hilo ili kuondoka naye lakini
mzazi mmoja aliona na kupiga kelele huku akilishambulia kwa mawe gari
hilo hadi walipomshusha mwanafunzi huyo na wao kutimka.
Maafande wa Kituo cha Polisi Buguruni wakiwa eneo la tukio kutuliza ghasia. WANAFUNZI WATOKA MADARASANI
Mayowe hayo yaliwafanya wazazi kuvamia shule hizo na kusababisha
wanafunzi kutoka madarasani huku wengine wakiruka ukuta na kukimbilia
majumbani na baadhi kwenda kusikojulikana.
Wazazi waliokuwa karibu na shule hizo walifika na kuwachukua watoto
wao kisha kwenda nyumbani huku wengine wakitegemea msaada toka polisi
ambao walipofika walifyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi hao.
Walimu wakipandishwa gari kurudishwa makwao. MANENO YA WALIMU
Hata hivyo, walimu wakuu wa shule hizo hawakupatikana mara moja
lakini mwalimu mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini
alisema hakuna utekaji wa watoto shuleni bali baadhi ya watu wamekuwa
wakivumisha habari hizo na hivyo kuwatia hofu watoto.
MADAI YA WATU
Baadhi ya watu walioongea na gazeti hili walisema kuwa, wana taarifa
mbaya kwamba watekaji hao wakishawapata watoto huenda kuwaua ili kutwaa
viungo vyao kwa ajili ya ushirikina wa kupata utajiri.
Baadhi ya walimu wakilindwa na maafande wasishambuliwe na wazazi waliovamie shuleni hapo. UONGOZI WA MTAA
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kombo, Jastin John Chiganga
alipohojiwa alikiri kutokea kwa vurugu hizo hali iliyomfanya awaite
polisi kutuliza ghasia lakini alisema kwa upande wa kutekwa watoto na
gari aina ya Noah hajawahi kusikia.
“Shule ilibidi ifungwe, watoto waruhusiwe kutawanyika hadi hapo
taarifa itakapotolewa. Hata hivyo, wazazi wameniomba kwamba kabla watoto
wao hawajarejea shuleni hapo anatakiwa kiongozi wa juu, awe DC (mkuu wa
wilaya) au yeyote afike kutoa tamko na kuweka mambo ili kuwatoa hofu
wazazi na wanafunzi,” alisema mwenyekiti huyo.
Mwanafunzi
Hadija Hansi (10) wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Magomeni, Dar
aliyepotea. Polisi wa Buguruni waliokuwepo kwenye tukio hilo walisema
hawana taarifa ya watu waliojeruhiwa au kukamatwa bali zoezi la
kudhibiti amani lilifanyika kwa uangalifu wa hali ya juu.
Wakati huohuo, wazazi wa mwanafunzi Hadija Hansi (10) anayesoma
darasa la nne Shule ya Msingi Magomeni, Dar wanahaha kumtafuta mtoto wao
huyo ambaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha ikidaiwa alitekwa
na Noah.
Mfano wa gari la Noah linaloshukiwa kuhusika na utekaji wa watoto Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita, Zena Amour ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo alisema mwanaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha Septemba 30, mwaka huu wakati akicheza na wenzake na ameshamtafuta katika vituo vya polisi jijini kikiwemo cha Tandale TAND/RB/1059/2014 na hospitali zote bila mafanikio.
0 maoni:
Chapisha Maoni