WALIOFARIKI KWA AJALI YA MOTO GEITA WAFIKIA WANNE!
Mkuu wa
Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie.
Watoto wengine waliotetekea katika ajali ya
moto huo, ni Reginald Robert (9), ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne na
Sofia (6) wa Shule ya Msingi Ukombozi na Remijius (4) wa Chekechea, walifariki
papo hapo.
Mkewe, Angelina akizungumza kwa shida
kutokana na kuondokewa na watoto wake wanne, alisema huo si msiba zaidi ya
msiba, kutokana na kubakiwa na watoto wawili kati ya sita, ambao wanne
wakifariki katika tukio hilo.
Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Wilaya, Dk. Adam Sijaona, alisema kuwapo kwa tukio hilo kumemfanya
akutane na mkasa, ambao hajawahi kukutana nao.
Afisa Mtendaji kata ya
Kalangalala, Hamad Hussein, alisema waliotenda tukio hilo walimimina mafuta ya
petroli milangoni na madirishani na kuilipua nyumba hiyo iliyoezekwa kwa bati
inawezekana kwa chuki binafsi ama migogoro ya ardhi.
Mwenyekiti wa Serikali
ya Mtaa huo, Hassan Mcharo na Afisa Mtendaji wa Mtaa huo, Simfukwe Ally, kwa
pamoja wamelaani tukio hilo wakati wakizungumza na gazeti hili juzi.
Mkuu wa Wilaya ya
Geita, Manzie Mangochie, akizungumza kwa masitikiko kuhusu tukio hilo, alisema
amesikitishwa na kitendo hicho na kuagiza kuhakikisha kuanzia ngazi ya mtaa
hadi wilaya wanashirikiana kuhakikisha waliohusika na unyama huo wanakamatwa.
Idadi ya watoto wa familia moja waliokufa
kwa ajali ya moto katika nyumba ya wazazi wao waliyokuwa wakiishi, mkoani
Geita, imeongezeka kutoka watatu hadi wanne, baada ya mmoja wao aliyekuwa
amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando, mkoani Mwanza, kufariki dunia.
Mtoto huyo, Scolastika
(15), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya
Mwatulole, alizikwa Septemba 14,2014.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari katika Kitongoji cha Elimu, Kata ya Kiangalala, mjini Geita, mara
baada ya kumzika mtoto wake wa nne, alisema ‘tulikiona kifo’.
Alisema
alimwambia mkewe, Angelina Gasper, wapige magoti na kuomba nusura ya Mungu
baada ya moto huo kuzuka katika nyumba wanayoishi.
Nyumba
hiyo iliteketezwa usiku wa Septemba 7, mwaka huu, baada ya watu
wasiofahamika kuimwagia mafuta ya petroli.
0 maoni:
Chapisha Maoni