Video
ya mauaji hayo ya kinyama inaanza kwa kuonyesha hotuba ya Waziri Mkuu
wa Uingereza David Cameron kuhusu Iraki, ikifuatiwa na ujumbe kwa
washirika wa Marekani dhidi ya kikundi hicho, na inahitimishwa kwa tukio
la kuogofya la kukatwa kichwa kwa Davidi ambaye ni Mskochi.
Tukio
hilo limetokea na kurekodiwa katikati ya jangwa. Baada ya hotuba ya
Cameron, mtu aliyejifunga kitambaa kuficha uso huku ameshikilia kisu
anaonekana amesimama mbele ya David ambaye amepiga magoti, na kuamriwa
kusoma ‘hotuba ya mwisho.’
Katika hotuba hiyo fupi, Mwingereza huyo anasema, namnukuu, “Ninapenda
kubainisha kuwa ninakulaumu Davdi Cameron kwa kuuawa kwangu.Umeingia
kwa hiari katika ushirika na Marekani dhidi ya Dola ya Kiislam, kama
alivyofanya mtangulizi wako Tony Blair.”
Baada ya kusoma taarifa hiyo, Davidi anakatwa kichwa kisha Mwingereza mwingine, Alan Henning anaonyeshwa akitishiwa maisha.Mtu aliyefanya uchinjaji huo anaonekana kuwa ni yuleyule aliyewachinja watu wengine wawili kabla ya tukio hili.
Kadhalika, anasikika akitoa onyo, namnukuu, “Iwapo wewe Cameron utaendelea kupambana na Dola ya Kiislam, basi wewe, kama bwana wako Obama, mikono yenu itakuwa na damu ya watu walio mateka wetu.”
0 maoni:
Chapisha Maoni