DA! Duniani kuna mambo jamani! Katika
hali isiyo ya kawaida, maeneo ya Tandale Kwatumbo jijini Dar, waombolezaji
hawakuamini macho yao wakati walipomuona ‘marehemu’ Mohamed Salum ‘Fido’ (29)
(pichani), akirejea nyumbani hapo huku maandalizi ya mazishi yake yakipamba
moto na waombolezaji, hasa mkewe, mtoto na ndugu wakilia kwa uchungu kufuatia
‘kifo’ chake.Kijana Mohamed Salum ‘Fido’ anayesadikiwa kuwa alikufa.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, mwaka huu, saa sita mchana wakati
shughuli mbalimbali za mazishi yake zikiendelea zikiwa ni pamoja na maandalizi
ya chakula cha mchana kwa waombolezaji.Iko hivi; Fido ni dereva wa bodaboda,
kijiwe chake kikiwa Lumumba Mnazi Mmoja, Dar. Inadaiwa kwamba Septemba 10,
mwaka huu alikamatwa na polisi wa ‘Tigo’, Lumumba kwa madai ya kutokuwa na
kibali cha kuingia mjini, akapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central).
Pale kituoni, habari zinadai maafande
hawakumruhusu kumpigia simu mkewe ili kumweleza yaliyompata, ndipo ndugu
walipoamua kumtafuta kwa siku mbili bila mafanikio.
kwa siku mbili bila mafanikio.
Waombolezaji
wakiwa msibani.
Septemba 11, mwaka huu, mkewe, kaka
yake na baba yake mzazi walikwenda Hospitali ya Mwananyamala na kuingizwa
chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) ambapo walioneshwa maiti moja! Vilio
vikaibuka kwani wote walisema ni Fido. Marehemu huyo aliuawa kwa kugogwa na
kitu kizito kichwani na maiti yake ilipelekwa hapo na polisi.
Ndugu hao walitoka na vilio hadi
nyumbani na msiba ukawekwa kwa kukusanya mikeka na chakula kuanza kupikwa huku
sehemu ya kuzikia makaburini ikitafutwa achilia mbali sanda kupatikana huku
ndugu walio mbali wakijulishwa kuhusu msiba huo.
Siku ya tukio, watu wakiwa katika
maandalizi ya mwisho kabla ya kuufuata mwili, ndipo Fido alipoibuka na
kusababisha tafrani kubwa.Baadhi ya watu waliingia mitini kwa woga huku ndugu
wakishangaa iweje maiti itoke mochwari yenyewe? Ndipo Fido alipotangaza kwa
sauti kuwa, hakufa, alikuwa polisi.
Kijana Mohamed Salum ‘Fido’
anayesadikiwa kuwa alikufa akila.
“Kweli sijui nisemeje, tuliwataka radhi
waombolezaji kwa usumbufu, baadhi walitawanyika kwa wakati huo wengine
waliendelea kuwepo hata ndugu zetu wengine wako njiani wakitokea Mbeya na
Mtwara.
0 maoni:
Chapisha Maoni