Rais wa Zamani wa Ukraine amesema kuwa mpango wa amani
umeafikiwa katika mazungumzo yanayolenga kusitisha mgogoro unaoendelea
mashariki mwa Ukraine.
Leonid Kuchma amesema kuwa mpango huo unahusisha kuwekwa kwa eneo la
kilomita 30 ambalo halitakuwa na majeshi kati ya mpaka wa ukraine na
Urusi,kuondolewa kwa vikosi vya kigeni mbali na kupigwa marufuku kwa ndege za
kijeshi zinazopaa katika eneo moja la anga ya mashariki mwa Ukraine.Bwana Kuchma amekuwa akifanya mazungumzo nchini belarus na wapiganaji wanaounga mkono Urusi ,balozi wa Urusi mjini Kiev Mikhail Zurabov pamoja na mjumbe kutoka shirika la usalama wa muungano wa ulaya.
Makubaliano ya kusitisha vita yalioafikiwa kati ya Ukraine na waasi hao mapema mwezi huu yamepunguza ghasia mashariki mwa Ukraine ,lakini kumekuwa na ripoti za ufyatulianaji wa risasai wa mara kwa mara na urushaji wa makombora kutoka pande zote mbili.
0 maoni:
Chapisha Maoni