MKUU WA MKOA SINGIDA DR.KONE
Uwakilishi wa majadiliano ya mkakati wa mkoa wa Singida
ilikuweza kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi kupitia taasisi au asasi za serikali na
zisizo za serikali zinapaswa kufikia malengo ya kupambana na gonjwa hilo.
Kauli hiyo imesemwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Perseco
Kone katika ukumbi wa Mikutano wa Kanisa la katoriki wakati akifungua mkutano
wa kujadili jinsi ya kupambana na maambikizi mapya ya ngonjwa la Ukimwi mkoani
Singida.
Dr. Kone amewataka wakilishi mbali mbali kutoka katika wilaya
zote za Singida kuwa makini na kile ambacho kitakacho amiwa katika mkutano huo
wa kujadili jinsi ya kupambana na gonjwa hatali la Ukimwi kwani maeneo yote ya
mkoa huu kunaongezeko la watu kwa kasi.
VIONGOZI KUTOKA MAENEO MBALI MBALI MKOANI SINGIDA.
Aidha Dr. Kone amesema kuwa mipango itakayo andaliwa ni vema
ikawa shilikishi kwa wadau mbali mbali
wa maeneo kwa hatua mbali mbali ili kuwa na uelewa wa pamoja na kufahamika kwa
shughuli ya aina moja kuwekewa nguvu zaidi kuliko maeneo mengine ya kupambana
na Ukimwi.
Watowa madaa katika mkutano huo.
Viongozi mbali mbali wa serikali na wasio wa serikali moani Singida wametakiwa kushilikiana na
wazazi na walezi ilikuweza kutowa elimu ya jinsia itakayo weza kuwasaidia
vijana katika kujitambua ilikuweza kupambana na gonjwa hatari la Ukimwi.
Dr.Kone amesema kuwa mafanikio ya Kikao ni kuhakikisha kile
ambacho kitaazimiwa katika mkutano huo lazima kifanyike kwa ufahasaha mkubwa
ilikuweza kufikia malengo yaliyo pangwa.
Aidha mkuu wa mkoa wa
Singida Dr. Kone ameeleza kuwa nivizuri ushirikiano na juhudi hizo za pamoja
zikaendelezwa kwani bado tuna safari ndefu ya kuhakikisha tunafanikisha malengo
tunayojipangia katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi na Ukimwi.
0 maoni:
Chapisha Maoni