MSANII WA MAREKANI T.I KUTUMBUIZA SERENGETI FIESTA DAR
Mkurugenzi
Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Ephraim Mafuru
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafala ya
kumtangaza msanii wa Marekani TI ambaye atashiriki tamasha la Fiesta
litakalofanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki
wa Kimarekani katika miondoka ya Hip-hop ambaye pia ni mtayarishaji wa
muziki, mwigizaji na mwekezaji, Clifford Joseph Harris Jr, alimaarufu
kama T.I. amethibitishwa rasmi na kampuni ya Serengeti Breweries Ltd
(SBL)kama mwanamuziki wa kimataifa atakayetumbuiza katika kilele cha
shangwe za Serengeti Fiesta zitakazofanyika jijini Dar es salaam tarehe
18 Oktoba mwaka huu.Katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya SBL, Meneja
Masoko Allan Chonjo alisema, ” hivi karibuni tumetia saini na
kukamilisha mikataba yote ili kuhakikisha kwamba mwanamuziki huyu wa
kimarekani anafika Leaders Club jijini Dar essalaam tarehe husika”
Chonjo
aliendelea kusema, ‘Tungependa kuwashukuru washirika wetu, Prime Time
Promotions kwa kuhakikisha tunakamilisha mikataba yote na vile vile kwa
kuhakikisha kamba tamaha hili linakamilika kwa mafanikio. Hii itakuwa ni
mara ya kwanza kwamba T.I kutia mguu wake katika ardhi ya Tanzania.
Akizungumza
na vyombo vya habari, Sebastian Maganga kutoka Prime Time Promotions,
alikuwa na haya ya kusema, “kwa miaka kadhaa sasa tumekuwa tukihakikisha
kwamba tunaelewa nini watanzania wanataka na tumekuwa tukijitahidi bila
kuchoka kuhakikisha kamba tukio tunalolifanya, kwa mwaka huu, wapenzi
wetu watashuhudia shoo ya nguvu ambayo haijawahi yanyika hapa nchini.
“mpaka
sasa, Serengeti imetembelea mikoa kumi (10) nchini, na itaendelea na
ziara hiyo katika mikoa ya Singida, Songea, Mtwara, Dodoma na Mbeya.
Mkurugenzi
wa Prime Time na meneja wa vipindi wa Radio Clouds FM Ruge Mutahaba
akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam kuhusu ujio wa mwanamuziki wa Marekani TI atakayeshiriki tamasha
la Fiesta litakalofanyika Dar es Salaam mwezi ujao.
Katika
mabadiliko mengine Serengeti Breweries na Prime Time Promotions
wamewaomba mashabikiwachague msanii wa kitanzania ambaye wangependa
atumbuize na TI. “Hiki ni kitu kipya natunataka kuhakikisha kwamba
mashabiki wanaburudika vya kutosha, alisema Maganga. ‘Habari
zitasambazwa kwa njia ya TV na redio kuelezea jinsi ya kushiriki’,
aliongeza.
Serengeti Fiesta inatambulika kwa kuleta wasanii wa kimataifa hapa
nchini, miongoni mwao ni pamoja na Rick Ross, Shaggy na Davido
T.I
aliyetamba na kibao “No Mediocre” amekuwa akijishughulisha na shughuli
mbalimbali ikiwemo biashara. Yeye ni muasisi na mkurugenzi mkuu wa Grand
Hustle Records.
T.I.
alianza kupata umaarufu mwaka 2003, baada ya kushirikishwa na
mwanamuziki mwenzake Bone Crusher, ambaye ni mkazi wa Atlanta, katika
wimbo wa “Never Scared”. Alipata umaarufu zaidi baada ya kutoa wimbo
wa Trap Muzik (2003).
Mwaka
2004, T.I. alionekana kwenye wimbo wa Destiny’s Child’s “Soldier”,
sambamba na Lil Wayne. Albamu ya sita ya TI, Paper Trail (2008), ilikuwa
albamu yake ya mafanikio zaidi , na imefanikiwa kuuza nakala 568,000
katika wiki ya kwanza nchini Marekani na kuifanya ya tatu katika chati
ya albam bora nchini humo. Mpaka sasa, T.I. amdeshinda tuzo tatu za
Grammy Awards.
T.I.
pia ametoa nyimbo kama vile”Bring Em Out”, “What You Know”, “Swagga
Like Us” (akimshirikisha Kanye West, Jay-Z and Lil Wayne), “Dead and
Gone” (akimshirikisha Justin Timberlake), “Ball” (akimshirikisha Lil
Wayne) and “No Mediocre” (akimshirikisha Iggy Azalea).
Mkurugenzi
Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Ephraim Mafuru (kushoto)
akimpongeza Mkurugenzi wa Prime Time Ruge Mutahaba wakati wa kumtangaza
mwanamuziki wa Marekani TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta mwezi ujao
jijini Dar es Salaam.Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Allan Chonjo akizungunza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakimtangaza mwanamuziki TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao.
Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Ephraim Mafuru (katikati) pamoja na Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rogamba (kushoto) na meneja masoko Allan Chonjo wakati wa kumtambulisha mwanamuziki wa Marekani TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Masoko ya Kampuni ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Prime Time Ruge Mutahaba ( wa tatu kushoto), meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo (wa pili kutoka kushoto), Elihuruma Ngowi (kushoto) na kulia ni meneja masoko wa Serengeti Allan Chonjo, wakati wakitangaza ujio wa mwanamuziki wa Marekani TI akayeshiriki katika tamasha la Fiesta litakalofanyika Oktoba 18 jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni