COASTAL UNION YAREJESHA FURAHA JANGWANI, WAING’ANG’ANIA SIMBA SC 2-2 TAIFA
Karate, au soka? Kiungo wa Simba SC, Ramadhani SIngano 'Messi' katikati ya wachezaji wa Coastal, Sabri Rashid kulia na Ayoub Yahya katika mchezo wa leo |
Mabao yote ya Simba SC inayofundishwa na Mzambia, Patrick Phiri akisaidiwa na wazalendo Suleiman Matola na Iddi Pazi ‘Father’ yalitokana na jitihada za mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Emmanuel Okwi.
Kisiga alifunga bao zuri la kwanza akimtungua Shaaban mwenzake, mtoto wa mzee Hassan Kado kwa mpira wa adhabu dakika ya sita, baada ya Okwi kuangushwa nje kidogo ya boksi.
Mfungaji bora wa msimu uliopita, Mrundi Tambwe akaanza msimu na bao kuashiria hataki kuvua ‘kiatu cha dhahabu’ baada ya kuunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya Mganda, Okwi dakika ya 36.
Coastal Union nao walipoteza nafasi mbili nzuri za kufunga kipindi cha kwanza, kwanza dakika ya tatu baada ya Mkenya, Itubu Imbem kuunganishia juu ya lango krosi ya Hamad Juma na baadaye Joseph Mahundi akashindwa kuunganisha krosi ya Mkenya huyo dakika ya 29.
![]() |
Bao la kwanza; Shaaban Kisiga akishangilia na Ramadhani Singano 'Messi' kushoto baada ya kufunga bao la kuongoza |
![]() |
Amisi Tambwe akimtoka beki wa Coastal, Mbwana Hamisi 'Kibacha' |
![]() |
Tambwe akishangilia baada ya kufunga bao la pili |
![]() |
Emmanuel Okwi akimkimbiza beki wa Coastal, Sabri Rashid |
0 maoni:
Chapisha Maoni