Alhamisi, 18 Septemba 2014

BASI LATUMBUKIA MTO PANGANI BAADA YA KUFELI BREKI

               BASI LATUMBUKIA MTO PANGANI BAADA YA KUFELI BREKI


Basi la la abiria kampuni ya SHAKILA lenye namba za usajili T 906 AJE linalofanya safari zake kati ya wilaya ya PANGANI na  TANGA MJINI limetumbukia majini  sehemu ya mbele baada breki kufeli.
Katika tukio hilo dereva wa basi hilo amejeruhiwa na pikipiki moja kutumbukia mtoni, huku abiria wote wa basi hilo wakielezwa kuwa salama.

 mwaka huu majanga basi lanusurika kuzama mto pangani Kwenye kivuko cha mv pangani baada ya kufeli break jana asubuhi majeruhi dereva peke yake


Tukio hilo limetokea LEO majira ya saa moja asubuhi wakati basi hilo likijaribu kuingia ndani ya kivuko cha MV PANGANI NAMBA MBILI likitokea KIPUMBWI kwenda  PANGANI MJINI, ndipo liliposhindwa kujihimili na kugonga pikipiki moja iliyozama na kusababisha sehemu ya mbele ya basi hilo kutumbukia majini.


Katika tukio hilo Pikipiki aina ya SAN LG yenye rangi nyekundu ambayo namba yake haikuweza kufahamika mara moja; imetumbukia mtoni baada ya kugongwa kwa nyuma na basi hilo ikiwa ndani ya kivuko cha MV PANGANI NAMBA MBILI, na taarifa za kiusalama zinasema kuwa bado pikipiki hiyo haijatolewa ndani ya maji.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: BASI LATUMBUKIA MTO PANGANI BAADA YA KUFELI BREKI Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top