BASI LATUMBUKIA MTO PANGANI BAADA YA KUFELI BREKI
Basi
la la abiria kampuni ya SHAKILA lenye namba za usajili T 906 AJE linalofanya
safari zake kati ya wilaya ya PANGANI na
TANGA MJINI limetumbukia majini
sehemu ya mbele baada breki kufeli.
Katika
tukio hilo dereva wa basi hilo amejeruhiwa na pikipiki moja kutumbukia mtoni,
huku abiria wote wa basi hilo wakielezwa kuwa salama.
Tukio
hilo limetokea LEO majira ya saa moja asubuhi wakati basi hilo likijaribu
kuingia ndani ya kivuko cha MV PANGANI NAMBA MBILI likitokea KIPUMBWI
kwenda PANGANI MJINI, ndipo liliposhindwa
kujihimili na kugonga pikipiki moja iliyozama na kusababisha sehemu ya mbele ya
basi hilo kutumbukia majini.
Baadhi
ya mashuhuda wamesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki ya gari
hiyo, hali iliyopelekea dereva kushindwa kuhimili basi hilo na kuamua kuruka
kabla ya sehemu ya mbele ya basi hilo kutumbukia katika mto huo.
Katika
tukio hilo Pikipiki aina ya SAN LG yenye rangi nyekundu ambayo namba yake
haikuweza kufahamika mara moja; imetumbukia mtoni baada ya kugongwa kwa nyuma na
basi hilo ikiwa ndani ya kivuko cha MV PANGANI NAMBA MBILI, na taarifa za
kiusalama zinasema kuwa bado pikipiki hiyo haijatolewa ndani ya maji.
si hilo kutumbukia majini.
0 maoni:
Chapisha Maoni