Jumatatu, 24 Machi 2014

Kamati kumi nambili zimetajwa  katika Bunge maalu la katiba  na  Mwenmyekiti wa Bunge  hilo Bw . Samwali Sita  ambapo kuwa na mabmbo mengi yametokera katika bunge hilo ambalo watanzania wataraji kupata muongozo wa taifa hili.



 Maneno mazuri ya hekima yaliyotolewa na Baba wa Taifa mwaka 1995. Tanzania imejaa Rushwa na watanzania wanatakiwa kupambana na rushwa. Tunataka mgombea URAIS ambaye hashiriki rushwa na atakayekemea Rushwa. Pili alikemea Ukabila na Udini. Alisisitiza suala la kuimarisha muungano, umoja, upendo na mashikamano. Je! Watanzania leo mna maoni gani juu ya kauli za baba wa taifa?je!
Yamepitwa na wakati? Mwakani ni uchaguzi je tunafikiria kumpata mgombea anayeyatambua na kuyakubali haya kuwa ndo kazi yake kuu ya kuijenga nchi na akapambana na rushwa? Je mnamfikiria mtu atakayelinda na kuimarisha utaifa na uzalendo na ambaye hatawaza kujiimarisha kiuchumi akiwasahau wanyonge na kuligawa taifa? Kazi kwetu watanzania kusuka au kunyoa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top