UKATILI:-Baba
amnyonga Mwanae mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba kisha kuacha
Ujumbe…..Tutafute Pesa kwanza J.M A.K.A GAIDI.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mbeya,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,AHMED Z.
MSANGI.
MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HENRY JUMA MKAZI WA MIGOMBANI ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA
SHINGO KISHA KULAZWA KITANDANI NA BABA YAKE MZAZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA JUMA VENANCE.
TUKIO HILO LA KUSIKITISHA LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014 MAJIRA
YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KATA YA MIGOMBANI, TARAFA YA TUNDUMA,
WILAYA YA MOMBA AMBAPO BAADA YA UHALIFU HUO, MTUHUMIWA ALIFUNGA MLANGO KWA NJE
NA KUFULI NA KUTOKOMEA MAHALI KUSIKOJULIKANA.
WAPELELEZI PAMOJA NA RAIA
WALIPOVUNJA MLANGO NA KUINGIA NDANI WALIKUTA MAITI YA MTOTO HUYO IKIWA
KITANDANI. KATIKA CHUMBA HICHO WALIKUTA UJUMBE WA MANENO MENGI YALIYOANDIKWA NA
MTUHUMIWA, BAADHI YA MANENO HAYO NI “UNYAMA UNYAMANI, TUTAFUTE PESA
KWANZA NIITE J.M A.K.A GAIDI”. JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE
0 maoni:
Chapisha Maoni