First eleven mpya ya Simba na Yanga
MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Bara unaelekea ukingoni huku kukiwa
na ushindani mkubwa kuwania nafasi tatu za juu baina ya timu za Azam,
Yanga, Mbeya City na Simba.
Kabla ya mechi ya leo Jumamosi itakayozikutanisha
Yanga na Mtibwa Sugar, Simba imecheza mechi nane za mzunguko wa pili
huku Yanga ikiwa imecheza mechi nne tu. Wapo wachezaji wenye majina
makubwa na ghali waliosajiliwa na Simba na Yanga lakini bado hawajafanya
lolote jipya kwenye mzunguko wa pili.
Timu ya Mwanaspoti imefanya tathmini ya utendaji
wa wachezaji mbalimbali wa Simba na Yanga uwanjani katika mechi za
mzunguko wa pili pekee na kupata kikosi cha kwanza cha mseto cha timu
hizo kongwe nchini kilichofanya vizuri mpaka sasa.
1. Deo Munishi ‘Dida’ (Yanga)
Kipa huyu alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu
huu akiwa amemkuta Ally Mustapha ‘Barthez’ akiwa namba moja baadaye
Desemba mwaka jana akawasili Juma Kaseja na kumwongezea changamoto ya
kucheza kikosi cha kwanza.
Kocha Hans Van Der Pluijm ameonyesha kumwamini na
kumpa nafasi akiwapiku Kaseja na Barthez kwani katika mechi kumi za
mashindano alizocheza, amefungwa mabao manne tu. Ameonyesha uimara
langoni kuliko hata Ivo Mapunda wa Simba.
2.Mbuyu Twite (Yanga)
Kiraka Mbuyu Twite ameonyesha uwezo mkubwa katika
kikosi cha Yanga, akicheza beki ya kulia kutokana na uwezo wake mkubwa
wa kuzuia na kupandisha mashambulizi huku akisaidia viungo katika
kuzuia.
Amekuwa msaada mkubwa kukaba na mabeki wa kati
pindi wanapofanya makosa. Twite ndiye mbadala wa kwanza katika beki ya
kati endapo Kelvin Yondani au Nadir Haroub ‘Cannavaro’ mmoja wao
asipokuwemo kikosini, mipira yake ya kurusha haitofautiani na mipira ya
kona.
3.Oscar Joshua (Yanga)
Beki wa kushoto Oscar Joshua wa Yanga hana vitu
vingi uwanjani kwani huwa anafanya kazi mbili tu za msingi, kukaba na
kupiga krosi za maana huku akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti
langoni.
Uwezo wake katika mzunguko wa pili umemshawishi
Kocha Pluijm kumpa nafasi kikosi cha kwanza na amekuwa akicheza mechi
nyingi za Yanga katika nafasi hiyo. Hana mchezo anapokuwa kazini.
0 maoni:
Chapisha Maoni