ZITTO KABWE ASISITIZA HANG'OKI CHADEMA, ASHUTUMU SLAA NA MBOWE KWA UBABAISHAJI
Sehemu ya wananchi wa mjini Kasulu waliojitokeza kusikiliza hotuba ya zito kabwe ambayo sehemu kubwa ilihusu kupinga kuvuliwa madaraka ndani ya chama chake pamoja na kuwataka wananchi kuungana kuwapinga viongozi wa Kamati kuu ya CHADEMA iliyowavua uongozi Zitto Kabwe, Dr. Kitilya Mkumbo na Migamba kwa tuhuma za Uhaini na usaliti kwa chama hichoZITTO KABWE aliyekuwa Naibu Katibu mkuu na naibu msemaji wa Kambi ya Uoinzani Bungeni (aliyevaa nguo za asili) Muda mfupi baada ya kuvalishwa mavani ya kitemi na wazee wa Heru juu katika JImbo la Kasulu Mjini, kabla ya kuanza kuwahutubia maelfu waliofurika uwanjani hapo. Mkutano huo uliandaliwa na kundi la viongozi wa CHADEMA jimbo ambao pia hivi karibuni wamefukuzwa uongozi na chama hicho ngazi ya wailaya kwa kile kinachotajwa kuwa ni kumuunga mkono ZItto na kupinga uamuzi wa kamati kuu
Viongozi wa Chadema kadhaa hasa wa ngazi za juu wilaya ya Kasulu hawakujitokeza katika mkutano huo.
Maelfu ya wakazi wa Mji wa Kasulu mkoani Kigoma wakimsikiliza mbunge wa Kigoma Kaskazini (aliyefukuzwa unaibu katibu mkuu wa Chadema) wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja ambapo Dr. Slaa alishambuliwa na wananchi wanaopinga kamati kuu ya chama hicho kumfykuza uongozi ZITTO
Moja kati ya mabango ya wnanchi ambao walikuwa kwenye mapozi ya mbunge wa jimbo la kigoma kasikazini Bw. Zitto wakati akiwa wilaya ya kasulu mkoani Kigoma
Na hayo nikati ya mengi yaliyokuwepo katika mapokezi ya mbunge huyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni