Jumatatu, 2 Desemba 2013

SOMA HAPA HABARI ZA MICHEZO HASA SOKA

      *MICHEZO 2DECEMBER2013*

Coastal baba lao Kombe la Uhai

Straika hatari afunga usajili Jangwani

Mkude amjia juu Poulsen

Yanga wamtisha Berko

COAST MABINGWA UHAI CUP

Saa 60 za mashaka makubwa kwa Wenger

Mastaa wanavyojipatia kadi za njano makusudi

==============================

COASTAL Union ya Tanga ndio vinara wapya wa michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu Bara.

Coastal imefanikiwa kulibeba taji hilo lililokuwa likishikwa na Azam baada ya kuibwaga Yanga mabao 2-0 katika fainali iliyochezwa jana  Jumapili kwenye Uwanja wa Azam, Chamanzi, Dar es Salaam.

Vijana wa Coastal waliandika bao la kwanza katika dakika ya 50 upitia kwa Mohammed Kipanga.

Kipanga alifunga akiunganisha krosi ya Abdallah Waziri. Kipa wa Yanga, Said

Coastal baba lao Kombe la Uhai

Ndutu, hakuona ndani, bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya aina yake na mashambulizi ya zamu kuliandama kila lango hadi ziliposalia dakika tatu mchezo kumalizika pale, Mahadhi Juma, alipoipatia Coastal bao la pili baada ya kuinasa pasi ya Mohammed Rajabu akiwa ndani ya 18.

Kibadeni awasifu vijana wake Simba

Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni ‘King’ amewasifu wachezaji wake vijana kwa kusema mchango walioutoa katika kikosi chake mzunguko wa kwanza ulikuwa mkubwa kuliko wa wakongwe.
Simba imehitimisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ikiwa imehifadhi pointi 24 na kukamata nafasi ya nne.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,Kibadeni alisema:
Watu wengi hawakuwa na imani na kikosi chetu hasa kutokana na kuwa na wachezaji wengi vijana,lakini ukweli ni kwamba mchango wao ndiyo ulikuwa mkubwa zaidi kuliko hata wakongwe, alisema Kibadeni na kuongeza:
Kama nilivyosema awali na leo narudia hii timu bado inaandaliwa,kama tutatwaa ubingwa sawa lakini hicho si kipaumbele changu kwa sasa.
Katika hatua nyingine, Kibadeni alisema, atatumia kipindi cha dirisha dogo la usajili kuisuka upya safu yake ya ulinzi baada ya kugundua baini kuwa ina upungufu.
Kuna upungufu katika safu ya ulinzi ambayo inatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wakati wa dirisha dogo la usajili,” alisema Kibadeni na kuongeza:
Hata katika nafasi ya kipa bado haijatulia sana utaona kuna mabao mepesi tunafungwa ndiyo maana niliamua kumpumzisha Abel Dhaira na kumtumia Abuu Hashimu ambaye naye utaona katika mechi tatu amefungwa mabao matatu.
Mzunguko wa kwanza umemalizika juzi Alhamisi na kwa Yanga kuongoza ligi hiyo kwa pointi 28 na kuzishusha Azam na Mbeya City katika nafasi ya pili na tatu wakiwa na pointi zao 27, huku Simba ikiwa nafasi ya nne.




Mkenya aacha kazi Yanga

Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu ya Yanga, Patrick Naggi ameacha kazi akidai ni kutokana na ubabaishaji wa viongozi wa klabu hiyo.
Naggi ambaye ni Mkenya amefikia uamuzi huo hivi karibuni baada ya kukaa muda mrefu bila ya kusaini mkataba wowote wa kuitumikia klabu hiyo tangu alipotua hapa nchini Septemba mwaka huu kwa ajili ya kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo.
Hata hivyo, hakuweza kupewa cheo hicho baada ya kuzuka kwa malumbano kati ya viongozi na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo ambao hawakutaka apewe nafasi hiyo ya Katibu Mkuu ambayo inakaimiwa na Lawrence Mwalusako.
Kutokana na hali hiyo uongozi wa Yanga ulimteua kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu kazi ambayo ameifanya kwa muda wa miezi mitatu bila ya kuwa na mkataba wa aina yoyote.
Akizungumza na gazeti hili jana, Naggi alisema kuwa kila alipokuwa akiuliza kuhusianana na mkataba wake viongozi wa klabu hiyo walikuwa wakimpiga chenga. “Ni kweli kabisa nimeamua kuachana na Yanga kwa sababu ya ubabaishaji wa viongozi wake, kwani tangu nimefika hapa nafanya kazi bila ya kuwa na mkataba na kila nikiuliza wanabakia kunipiga kalenda.
Wakati nakuja Yanga waliniambia nakuja kuwa Katibu Mkuu lakini baada ya kufika mambo yakabadilika wakaniambia niwe Mkurugenzi wa Ufundi kwa sababu tu nina uzoefu na kazi hiyo kutokana na kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Ligi ya Soka ya Kenya (FKL) hapo awali kabla ya kujiunga na klabu hiyo.
“Nilikubali kuchukua nafasi hiyo na wao wakaanza mikakati ya kuniandalia mkataba na kilichokuwa kimebakia ni mimi kupiga dole gumba lakini dakika za mwisho wakawa hawaeleweki na kila nikiuliza wananipiga kalenda, hivyo nimeona ni bora niachane na kazi hiyo nirudi kwetu nikaendelee na mambo yangu mengine,” alisema Naggi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alipoulizwa juu ya suala hilo aligoma kulizunguzia kwa madai kuwa lipo juu ya uwezo wake.
na kutoa maelekezo kuwa mwenye uwezo wa kulizungumzia ni Makamu Mwenyekiti, ClementSanga au Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji .
Wambura ajitosa Simba


Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) sasa TFF, Michael Wambura amejitosa kuvalia njuga mgogoro wa Simba unaoendelea na kudai kuwa amekubaliana na uteuzi wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba aliyoteuliwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage.
Akizungumza Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi, jana, Wambura alisema kwa mujibu wa Katiba ya Simba Ibara ya 28(1)(d) Mwenyekiti anaweza kuteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ya Simba bila kutoa nafasi ya wateuliwa kuuliza wameteuliwa kutoka katika kundi lipi kati ya wajumbe wawili.
“Nadhani jambo muhimu la kuhoji ni wanaoteuliwa wanakwenda kufanya nini kwenye Kamati ya Utendaji kwa maana ya uwezo wao kuisaidia Simba na sio nani ateuliwe na nani asiteuliwe kwani hilo liko katika mamlaka ya mteuzi ilimradi tu anayeteuliwa ni mwanachma wa Simba na ataongeza tija kwa klabu, alisema Wambura.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Wambura imepingwana Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Swedy Nkwabi ambaye alidai kuwa uteuzi wa Wambura kikatiba sio sahihi na kumshangaa Wambura kuzungumzia mgogoro wao wakati hawakukubaliana naye.
He! Yaani alituuliza kumbe lengo lake lilikuwa ni kuongea na vyombo vya habari, mimi nilijua ameuliza tu kutaka kufahamu na nilichukulia ushauri wake kuwa ni mzuri ila sikufahamu lengo lake hasa ni nini, nasemaje uteuzi wake kikatiba si sahihi na wala hatukubaliani na uteuzi huo, na pili nitakutana na wenzangu kuzungumzia jambo hili na tutalitolea tamko,” alisema Nkwabi.
Ninaamini uzoefu wangu katika uongozi wa mpira wa miguu na elimu yangu ulifaa kuingia katika Kamati ya Utendaji ya Simba, alisema Wambura.
Nilipata nafasi ya kuongea na Mwenyekiti  wa Simba na kisha kuongea na mjumbe mmoja mmoja wa Kamati ya Utendaji ili kujua kiini na sababu za sintofahamu iliyokuwa inaendelea ndani ya uongozi wa Simba, wajumbe walikuwa na masikitiko na manung’uniko ya msingi ambayo Mwenyekiti atakaporejea atakutana na kamati yake ili mamabo ya msingi yaliyozungumzwa yafanyiwe kazi na kupanga utekelezaji wake. Mwenyekiti ameisha taarifiwa juu ya auamuzi huu,” alisema
Ethiopia yaiumbua Zanzibar

Ethiopia imeipa Zanzibar kipigo ambacho kimefunua udhaifu wa timu hiyo ambao ni kukosa uzoefu, kutokujiamini na umakini finyu wa wachezaji wanaocheza ligi isiyo na ushindani wa kutosha.
Kipigo cha mabao 3-1 ilichopata Zanzibar jana kwenye Uwanja wa Nyayo kimeifanya kushindwa kujihakikishia nafasi ya kucheza robo fainali ya michuano ya Chalenji ikitokea Kundi A lenye wenyeji Kenya na Sudani Kusini.
Bao la kwanza la Ethiopia lilifungwa na Fasika Afsan dakika ya tano baada ya kupiga shuti lenye kilo nyingi lililomshinda kipa Abdallah Rashid lakini dakika ya 37 kiraka Salahadin Bargicho alifunga bao jingine kwa penalti baada ya beki Mohamed Faki kumkwatua Manaye Fantu aliyekuwa na madhara.
Bao pekee la Zanzibar ambayo si mwanachama wa Fifa, ambalo lilikuwa la kideo lilifungwa na Awadhi Juma kwa kichwa cha aina yake akiunganisha krosi ya Seif Abdallah dakika ya 68. Vijana hao wa Zanzibar walithibitisha kutokuwa na umakini pamoja na kutojiamini baada ya mabeki wake kumwacha Yonathan Kadebe akipiga kichwa mara mbili mbele ya lango na kufunga goli la tatu la Ethiopia dakika ya 84.
Mashabiki wa Ethiopia wamekuwa wakijazana uwanjani hapo kuliko wa timu nyingine yoyote ukiondoa wenyeji, Kenya.
Katika mechi nyingine jana, Kenya iliichapa Sudan Kusini mabao 3-1.

Ethiopia yaiumbua Zanzibar
Nairobi. Ethiopia imeipa Zanzibar kipigo ambacho kimefunua udhaifu wa timu hiyo ambao ni kukosa uzoefu, kutokujiamini na umakini finyu wa wachezaji wanaocheza ligi isiyo na ushindani wa kutosha.
Kipigo cha mabao 3-1 ilichopata Zanzibar jana kwenye Uwanja wa Nyayo kimeifanya kushindwa kujihakikishia nafasi ya kucheza robo fainali ya michuano ya Chalenji ikitokea Kundi A lenye wenyeji Kenya na Sudani Kusini.Bao la kwanza la Ethiopia lilifungwa na Fasika Afsan dakika ya tano baada ya kupiga shuti lenye kilo nyingi lililomshinda kipa Abdallah Rashid lakini dakika ya 37 kiraka Salahadin Bargicho alifunga bao jingine kwa penalti baada ya beki Mohamed Faki kumkwatua Manaye Fantu aliyekuwa na madhara.

Kili Stars yaipiga Somalia, kina Samatta, watua Kenya


KILIMANJARO Stars imeingiza mguu mmoja kwenye robo fainali ya Chalenji baada ya kuichapa Somalia 1-0 lakini Kim Poulsen amecharuka na kuwaita kikosini Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Poulsen ametangaza hali ya hatari kwenye mechi zijazo ikiwemo dhidi ya Burundi keshokutwa Jumatano mjini Nakuru na kusisitiza hakuna masihara tena kuanzia sasa kwavile mafowadi waliopo  wameshindwa kuonyesha makali.

Bao pekee la Kili Stars lilifungwa na Haruna Chanongo dakika 57 akipokea krosi ya Ramadhani Singano ‘Messi’.

Matokeo hayo ni tofauti na msimu uliopita ambao Stars ikicheza na Somalia tarehe kama ya jana Jumapili iliifunga mabao 7-0.

Kim alisema: “Katika mechi mbili tulizocheza dhidi ya Zambia na Somalia hakuna straika aliyefunga, ni kiungo na beki. Hii inamaanisha bado sisi si hatari kwenye ushambuliaji.”

“Nimewaita mastraika Samatta na Ulimwengu watatua leo (jana Jumapili) jioni na kuanzia mechi na Burundi tutakuwa hatari. Kwenye hizi mechi zilizopita fowadi yangu haikuwa na madhara jambo ambalo linafanya tufunge magoli machache na mepesi.

“Hatukuwa na madhara kwa mabeki, lakini ninaamini kwa ujio wa Samatta na Ulimwengu tutafanya mabadiliko makubwa kwavile wana uzoefu mkubwa na ni wachezaji ambao wamezoea mashindano, tutakuwa na madhara sana kuanzia mchezo ujao, hilo ndilo ninaloweza kuwathibitishia,” alisisitiza kocha huyo ambaye anaitumia michuano hiyo kuisuka timu kwa fainali za Afrika mwakani.

Katika mechi dhidi ya Somalia, Stars ilitengeneza nafasi nyingi lakini ikashindwa kumalizia huku wapinzani wao wakicheza kwa kukamia na kukaba kitimu tofauti na misimu iliyopita.

Stars ilichezesha kikosi chenye badiliko moja tu ya kile kilichotoka sare ya bao 1-1 na Zambia mjini Machakos. Katika kikosi cha jana Poulsen alimuweka benchi Hassan Dilunga na kumuanzisha Athuman Idd katikati akicheza na Frank Domayo.

Stars ilikuwa hivi; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Aboubakary Salum, Athuman Idd, Mrisho Ngassa/Mussa Shah, Elius Maguri/Chanongo na Amri Kiemba/Ramadhani Singano.

Kukamia kwa Somalia kuliwachanganya wachezaji wa Stars ambao walionekana kupaniki, ingawa kipindi cha pili Mussa Shah, Chanongo na Messi walibadili mchezo na kwenda sawa na vijana wa Somalia ambao fowadi yao ilikuwa butu.

Uwanja uliokuwa chepechepe ulikuwa kikwazo cha Stars kuonyesha mchezo mzuri ingawa pointi nne zimeipa faida ya kunusa robo fainali.

Straika hatari afunga usajili Jangwani

YANGA ina nafasi moja tu ya kusajili na hadi sasa viongozi wanakuna vichwa kuhusu nani asajiliwe na kwa nafasi ipi kati ya straika au beki wa kushoto atakayemudu kucheza winga pia.

Ingawa Yanga ina mastraika wengi lakini upo uwezekano mkubwa wa kuongeza straika mwingine wa maana kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika na hata kwa ajili ya Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

Mastraika waliopo kwa kiasi kikubwa wameonekana bado hawana kiwango ambacho Kocha Mkuu, Ernest Brandts anakitaka.

Brandts kila mara amekuwa akilalamikia washambuliaji wake kutokuwa makini na kukosa mabao ya wazi na aliwahi kupendekeza atafutwe straika mmoja wa maana hasa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.

Yanga ina mastraika sita ambao ni Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerry Tegete, Shaaban Kondo, Said Bahanuzi na Hussein Javu.

Kati ya hao Kiiza, Kavumbagu na Tegete ndio wamekuwa wakipata nafasi ya kucheza mara kwa mara wakati wengine waliobaki wamekuwa wakisugua benchi na wengine kugeuka watazamaji jukwaani.

Kiiza ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao ndani ya timu hiyo, amefunga mabao manane akifuatiwa na Kavumbagu na Tegete waliofunga mabao matano kila mmoja.

Brandts aliliambia Mwanaspoti kuwa kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa upande wa washambuliaji na hilo ndio analolipa mkazo katika usajili wa nafasi iliyobaki.

Washambuliaji ninao wengi lakini bado hawajaweza kucheza na kufunga mabao katika kiwango ninachotaka hivyo katika eneo hilo nahitaji kuongeza nguvu hasa kwa ajili ya mashindano makubwa ya kimataifa,” alisema Brandts.

Kikosi cha Yanga kina wachezaji 27 mmoja akiwa ni Omega Seme anayecheza kwa mkopo Prisons ya Mbeya na kwa mujibu wa TFF, timu haipaswi kusajili kwa pengo la mchezaji aliyepelekwa kwa mkopo.

Kwa maana hiyo,Yanga katika usajili huu mdogo ina nafasi ya kusajili wachezaji watatu tu, na tayari imeshawasajili wawili; kipa Juma Kaseja na kiungo Hassan Dilunga hivyo wamebakiwa na nafasi moja.

Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto aliliambia Mwanaspoti kwamba, wana nafasi moja tu ya kusajili ambayo hata hivyo uongozi bado unapambana kuhakikisha wanasajili mchezaji atakayeisaidia timu.




Mogella awacharukia mabosi Simba

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Zamoyoni Mogella amewalaumu viongozi wa Simba baada ya kutangaza kumleta kwa lengo la kumsajili aliyekuwa kipa wa Yanga, Yaw Berko.

Simba imemtumia tiketi ya ndege kipa huyo kutoka Ghana na alitarajiwa kuwasili jana Ijumaa saa tano usiku.

Mogella aliliambia Mwanaspoti kuwa anawashangaa Simba kwa uamuzi huo hasa kutokana na usumbufu ambao kipa huyo atawasababishia kutokana na majivuno aliyonayo licha ya kuwa na kiwango kikubwa uwanjani.

Alisema anadhani kipindi hiki timu hiyo ingekaa na kujipanga huku ikiwapa nafasi makipa waliopo na kuepuka kuongeza usumbufu kutokana na kuwa kwenye mgogoro wa uongozi.

“Alikuwepo kipa Ally Mustapha ‘Barthez’, akasota benchi misimu miwili, lakini ameenda Yanga ameonyesha uwezo na kuaminiwa, sasa kuna haja gani ya kuacha kuwaamini hao waliopo na kuongeza tatizo juu ya tatizo alisema Mogella.

Aliongeza: Nadhani timu yangu ya Simba ni kama wamechanganyikiwa, badala ya kufanya mambo ambayo yataleta utulivu na kujipanga kwa msimu ujao wanaleta kipa mpya ambaye ni mwinyi, anachagua mechi, hana adabu, kwa kuwa sifa za mchezaji ni kupambana hasa timu inapomuhitaji, mchezaji huyu hana hiyo sifa kwenye mechi ngumu ndiyo anasumbua.

Mogella pia aliiponda Kamati ya Utendaji ya Simba kwa kumtupia virago Kocha Mkuu Abdallah ‘King’ Kibadeni na kudai kuwa walichofanya ni unyama na udhalilishaji mkubwa.

Alisema kwa kikosi cha Simba cha sasa ilibidi Kibadeni apewe nafasi akisuke vizuri kwa ajili ya mafanikio ya baadaye kwani timu hiyo haikufanya vibaya kiasi cha uongozi kumtimua kama mbwa.

“Sidhani kama Kibadeni alirudi Simba kwa ajili ya fedha, ninachoamini alikuja kwa mapenzi na hiyo si mara ya kwanza, amewahi kuifanyia makubwa timu hiyo, alikuwa na timu ya Kagera ametulia wakaona alichokifanya wakamwita kwa kuwa alikuwa na mapenzi akawakubalia sasa hata hajafanya walichomuitia wanamtimua kama kocha wa mchangani, inasikitisha, wamemdhalilisha bila kuangalia amewahi kufanya nini katika klabu hiyo alisema Mogella.


    Zilizosomwa Sana

    Straika hatari afunga usajili Jangwani
    Mogella awacharukia mabosi Simba
    Yanga wamtisha Berko
    Kili Stars yaipiga Somalia, kina Samatta, watua Kenya
    Kocha Simba aja na dawa ya Yanga
    Kocha amchomoa kikosini Mbuyu Twite
    Ivo Mapunda ametupa somo la kipekee
    Diamond awataja mademu zake wanne, lakini anampenda huyu
    Saa 60 za mashaka makubwa kwa Wenger
    Mkude amjia juu Poulsen
    Manchester United majanga



    Habari Mpya

    Bausi ni deiwaka Zanzibar Heroes
    Matola: Simba, Yanga badilikeni
    Chuji atangaza kustaafu na rekodi
    Zanzibar Heroes yasaka sare
    Mkude amjia juu Poulsen
    Berko: Yanga kwangu ni historia
    Kocha amchomoa kikosini Mbuyu Twite
    Coastal baba lao Kombe la Uhai
    Manchester United majanga
    Kili Stars yaipiga Somalia, kina Samatta, watua Kenya

Yanga wamtisha Berko

WASHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi Didier Kavumbagu na Jerry Tegete, wameiambia Simba kwamba hata ikimleta kipa, Yaw Berko, kikosini mwao wao watamtungua tu kwa sababu wanajua ubora na upungufu wake.

Berko, kipa wa zamani wa Yanga, alitarajiwa kutua saa tano usiku wa jana Ijumaa akitokea kwao Ghana ili kumalizana na Simba kwa ajili ya kusaini kuwachezea Wana Msimbazi hao katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakizungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti, mastraika hao ambao mara nyingi hucheza kikosi cha kwanza cha Yanga chini ya kocha, Ernest Brandts, walisema hawamhofii Berko kwani wanajua kila kitu kuhusu yeye.

Tegete alisema: Berko ni kipa mzuri, lakini pamoja na ubora wake kwetu atafungika tu. Unajua tumekaa na Berko muda mrefu, ni yule yule hata hivyo hana tofauti sana na wengine kwani idadi kubwa ya makipa wanaocheza Ligi Kuu wanafanana.

Naye Kavumbagu alisema: Namfahamu Berko vizuri sana, kweli ukiwataja makipa imara na yeye ni mmoja wao, hivyo atawasaidia Simba, lakini kwangu mimi hanitishi nitamfunga tu kwani najua upungufu wake na ubora wake. Tutakapopambana nao itakuwa kazi rahisi kwangu kumfunga.
Kocha amchomoa kikosini Mbuyu Twite
HAKUNA jinsi kiraka wa Yanga, Mbuyu Twite, anaweza kurejea kwenye timu ya Taifa ya Rwanda katika siku za hivi karibuni.

Kocha wa Rwanda, Eric Nshimiyimana, amesema hana mpango na mchezaji huyo baada ya kumwita kwenye mechi dhidi ya Mali akakaidi na kuzima simu.

Nilimwita kwenye mechi dhidi ya Mali akagoma na simu akazima, hakuna jinsi nchi kubwa kama Rwanda inaweza kumnyenyekea mchezaji mmoja, alisema kocha huyo aliyeko mjini hapa kwenye mechi za Kombe la Chalenji.

“Ni tabia mbaya kwa mchezaji kuitwa na kukaidi, kocha hawezi kumnyenyekea mchezaji mmoja kwenye timu ya Taifa. Nafasi ya Mbuyu imeshazibwa na vijana wadogo ambao wanafanya kazi kikamilifu. “Hatuwezi kuendelea kuendekeza hizo tabia, tuna wachezaji kama wanne wadogo ambao wanaweza kufanya kazi vizuri kabisa, hakuna haja ya kuangaika na Mbuyu.

Rwanda iko kwenye kipindi cha mpito cha kusuka kikosi kipya cha wachezaji wengi wa ligi ya ndani kujiandaa na michuano ya Afrika miaka ijayo.

Mkude amjia juu Poulsen

KIUNGO Jonas Mkude aliyetemwa Kilimanjaro Stars kwa madai ya utovu wa nidhamu ameibuka akidai anamshangaa Kocha Kim Poulsen kwa kuwa kigeugeu.

Muda mfupi baada ya kumuacha Mkude katika kikosi cha Kili Stars, Poulsen alinukuliwa akisema amemwacha kutokana na utovu wa nidhamu hasa kuchelewa kambini kila anapoitwa licha ya kumuonya mara kadhaa lakini alishindwa kubadilika.

Mkude anayeichezea Simba aliliambia Mwanaspoti kuwa alishangaa kocha huyo kutoa madai ya utovu wa nidhamu kwani alipomuacha hakumueleza sababu hiyo na hata siku moja hajawahi kuwa mtovu wa nidhamu katika klabu na timu ya Taifa.

Aliponiacha katika kikosi aliniambia siwezi kucheza kwa kuwa ana viungo wengi wanaocheza vizuri zaidi yangu, akaniambia niendelee kujituma ili niweze kucheza alisema.

Sasa anaposema mimi mtovu wa nidhamu simuelewi, maana kama kuchelewa kambini niliomba ruhusa kwamba nina matatizo ya kifamilia, nilimuomba ruhusa meneja (Taso Mukebezi) na nilieleweka,” alisema Mkude.

Mkude aliitwa katika kikosi cha pili cha Taifa Stars, Future Young Taifa Stars pia alichaguliwa Taifa Stars iliyocheza mechi ya kirafiki naZimbabwe lakini akatemwa Kili Stars.

Viungo wa Kili Stars waliomnyima nafasi Mkude ni Amri Kiemba, Athuman Idd Chuji’, Frank Domayo, Haruna Chanongo, Hassan Dilunga, Ramadhan Singano na Salum Abubakar ‘Sure Boy.

Wadau wengi wa soka walishangaa kuachwa kwa Mkude na kupewa nafasi hiyo Kiemba licha ya ukweli kwamba Mkude alicheza kwa kiwango cha juu mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara akiwa na Simba.
              KIMATAIFA

Saa 60 za mashaka makubwa kwa Wenger

ARSENAL imejinafasi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England, imefanya hivyo baada ya kukusanya pointi 31 katika mechi 13 ilizotia timu uwanjani.

Kitendo hicho kinawafanya mashabiki wake kuanza kuzungumzia ubingwa hasa kutokana na kiwango kinachoonyeshwa na timu yao  msimu huu. Timu imekuwa ikishinda mechi zote zilizoonekana zingekuwa kikwazo kwao.

Pamoja na kuongoza ligi kwa pointi nyingi hasa dhidi ya mabingwa watetezi Manchester United, jambo hilo halimfanyi kocha wake,  Arsene Wenger, kuanza kupiga soga za kutwaa ubingwa. Kuna kitu kinamnyima raha Mfaransa huyo.

Wenger amechukia, kisa ratiba inayomkabili kwa sasa. Mfaransa huyo anaamini ratiba ngumu iliyo mbele yao itatibua mbio zao katika kufukuzia ubingwa wa msimu huu.

Vinara hao watakwenda kucheza ugenini na Manchester City ikiwa si zaidi ya siku tatu baada ya kucheza na Napoli, ambayo ni mechi ngumu ya kutafuta kufuzu hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa  Ulaya.

Kwenye mechi hiyo kama Arsenal itakubali kichapo cha mabao 3-0 basi itakuwa imetupwa nje ya michuano kitu ambacho Mfaransa huyo hataki kitokee.
Manchester United mbona
 Majanga
MSIMU wa shida Manchester United. Hicho ndicho unachoweza kusema baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England kuporomoka hadi nafasi ya nane kwenye msimamo kutokana na sare ya mabao 2-2 waliyoipata jana Jumapili dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye Uwanja wa White Hart Lane.

Mabao mawili ya straika, Wayne Rooney, yalishindwa kuinusuru timu hiyo walau kupanda nafasi za juu kwenye msimamo huo baada ya sare hiyo kuwafanya kufikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi 13. Hata hivyo, kikosi hicho kinachonolewa na David Moyes, kinaweza kushukuru kuambulia pointi hiyo moja ya ugenini baada ya mabao yake hayo iliyoyapata kwa kusawazisha.

Tottenham ilitangulia kwa bao la mpira wa adhabu uliopigwa na Kyle Walker kabla ya Sandro kufunga kwa shuti kali akiwa umbali wa mita 25.

Rooney alifunga bao lake la kwanza kwenye mchezo huo akitumia makosa ya beki Walker aliyeshindwa kuokoa krosi ya Phil Jones, wakati lile la pili lilitokana na mkwaju wa penalti iliyosababishwa na kipa Hugo Lloris kumwaangusha Danny Welbeck kwenye eneo la hatari.

Baada ya sare hiyo, Manchester United itakuwa na mtihani mgumu keshokutwa Jumatano itakapokuwa Old Trafford kuikaribisha Everton.

Mastaa wanavyojipatia kadi za njano makusudi

WANASOKA mahiri wamekuwa wakiendelea kujipatia kadi za njano kijanja kwa ajili ya kukosa mechi wanazoziona kuwa si muhimu. Ni kadi ambazo zinapikwa na watu wa benchi la ufundi kwa makusudi.

Yaya Toure vs Viktoria Plzen

Katika pambano la Jumatano usiku la Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya  Viktoria Plzen, Yaya, alicheza rafu ya kizembe makusudi katika dakika ya 92 dhidi ya Roman Hubnik.

Kinachoonekana ni kwamba lengo lake lilikuwa ni kuhakikisha kuwa anamaliza adhabu ya kutumikia kadi mbili za njano ili isimtibulie katika mechi za mtoano kwa sababu tayari Manchester City imeshapita.

Yaya alikuwa ameingia uwanjani katika dakika ya 65 wakati mechi ikiwa sare ya 1-1 na akapika bao la pili lililofungwa na Samir Nasri. Hata hivyo dakika ya mwisho ya mchezo alifanya hivyo rafu ya kijinga makusudi ili akose pambano la mwisho la makundi dhidi ya Bayern Munich akihofia kwamba kama angeenda katika mechi za mtoano akiwa na kadi ya njano huenda angekosa mechi muhimu zaidi.

KWA UFUPI TU KATI YA YALE AMBAO NIMEKUJUZA LEO.

Coastal baba lao Kombe la Uhai

Straika hatari afunga usajili Jangwani

Mkude amjia juu Poulsen

Yanga wamtisha Berko

COAST MABINGWA UHAI CUP

Saa 60 za mashaka makubwa kwa Wenger

Mastaa wanavyojipatia kadi za njano makusudi


             ……………………………………………..Mwisho……………………………………………
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: SOMA HAPA HABARI ZA MICHEZO HASA SOKA Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top