Kenya bingwa wa Challenge Cup 2013
Michuano
ya GoTv Senior Cecafa Challenge Cup imefikia mwisho wake hii leo kwa
mchezo wa fainali uliowakutanisha wenyeji The Harambee Stars ya Kenya na
timu ya taifa ya Sudan maarufu kwa jinal la Utani la The Falcons .
Katika mchezo huo Kenya ilifanikiwa kubakisha kombe hilo nyumbani kwa kuwafunga Sudan 2-0 .
Mabao yote mawili yalifungwa na mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo Allan Wanga ambaye huchezea klabu ya Fc Leopards .
Kabla
ya mchezo huo wa fainali kulikuwa na mchezo wa kuwania nafasi ya
ushindi wa tatu ambapo Timu ya taifa ya TANZANIA BARA ilishika nafasi ya
nne baada ya kufungwa na Zambia kwa mikwaju ya Penati .
Mchezo
huo uliisha kwa sare ya 1-1 baada ya Zambia kufunga kupitia kwa Ronald
Kampamba huku Tanzania ikisawazisha kupitia kwa Mbwana Samatta .
Katika
Mikwaju ya penati , Mrisho Ngassa, Haruna Channongo na Kelvin Yondani
walikosa penati zao na kuipa Zambia ushindi wa tatu . Fainali
inayowakutanisha Sudan na Wenyeji Kenya itapigwa saa 12 jioni .
Hii
ni mara ya kwanza kwa Kenya kutwaa ubingwa huo baada ya kuukosa kwa
miaka 11 tangu walipotwaa mara ya mwisho mwaka 2002 wakiwafunga Tanzania
Bara huko Mwanza kwa matokeo ya 3-2 .
Historia
nyingine iliyowekwa na Harambee Stars ni ile ya kutwaa taji hilo kwenye
ardhi ya nyumbani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1983 ilipowafunga
Zimbabwe 1-0.
0 maoni:
Chapisha Maoni