Ijumaa, 15 Novemba 2013

Kuhusu ishu ya uhamisho wa Emmanuel Okwi, kauli ya TFF iko hapa




Ishu ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi ambae aliuzwa na klabu yake ya Simba ya Dar es salaam kwa Etoile Sportif du sahel ya Tunisia bado inaendelea kuchukua headlines.

Inatokana na mshambuliaji huyu sasa hivi kuruhusiwa na mamlaka kuu za soka duniani (FIFA) kuchezea club yake ya zamani ya Villa ya Uganda wakati ambao bado club yake ya Simba haijalipwa hata shilingi moja na waarabu hao wa Tunisia.

Mamlaka husika za soka Uganda zilipambana kwa faida ya mchezaji na taifa la Uganda kuhakikisha mshambuliaji huyu hakai bure baada ya kurejea kwa kile alichokisema kwamba ni kulimbikizwa mishahara yake kwa muda mrefu bila malipo.

TMS manager wa shirikisho la soka Tanzania TFF Saad Kawemba amezungumza kuhusu ushiriki wao kama shirikisho kuzisaidia club za Tanzania hasahasa hii ishu ya Simba kushindwa kupata haki yao juu ya mauzo ya Okwi na kusema ‘tayari nimeona Simba wameandika barua na sisi tutaipitisha iende moja kwa moja kwenye player status committee ili waione hiyo kesi, hizo ndio documents ambazo zinakwenda zikisema hawa watu waliahidi kufanya hivi na hawajafanya hivyo tunaomba sasa walazimishwe kufanya hivi’

Kiukweli kabisa tunahitaji kuwa wavumilivu nadhani watu wanaweza kudhani kiongozi flani kafanya hivi, kakosea kachukua kitu flani na nini…… hapana, kwa sababu katika transfer inaonekana kwenye system wale hawajalipa, nizungumze jambo moja ambalo liko wazi kwenye system ni kwamba pale club mbili zinapokubaliana kuuziana mchezaji, mchezaji anaruhusiwa kwenda kwenye club mliyokubaliana na malipo yatafata baadae, kutokuwepo kwa malipo hakumzuii mchezaji kuhama… hiyo ni kanuni ya kwanza ya uhamisho’ – Kawemba

Kwa faida ya watu wote ni kwamba sisi hapa nyumbani tumezoea kabisa mchezaji hawezi kutoka mpaka nilipwe lakini kwenye mpira duniani ni kwamba mnakubaliana alafu pesa zinalipwa kidogokidogo, tunaomba watu wawe wavumilivu kwasababu tayari kesi iko mikononi mwa FIFA walikua nayo toka mwanzoni wakaomba Simba waongee na Tunisia na kweli walikwenda na kukubaliana ila hayajatekelezwa’ – hayo ni maneno ya Kawemba akiongea na sports Extra ya Clouds FM.

Kesi ya Simba iko wazi kabisa mbele ya FIFA na tunaamini kabisa kwamba Simba watanufaika na kesi hiyo kwa sababu hawajafanya kosa lolote kwenye uhamisho huo, nguvu yetu ni kuhakikisha kesi hii tunaishinda na club yetu inapata haki yake’ hii ni sentensi nyingine ya Kawemba unaeweza kumsikiliza hapa chini pia



  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top