Ijumaa, 15 Novemba 2013


                                   KWA KUANDFALIWA NA BANDOLA

ateua jeshi kuivaa Harambee Septemba 19


KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen, ameteua kikosi cha nyota 32 kuelekea mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya, Harambee Stars, itakayochezwa Novemba 19, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini  Dar es Salaam.
Katika kikosi hicho, Kim amewajumuisha wachezaji 16 kutoka Taifa Stars iliyo chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager na wengine 16 kutoka kikosi cha pili cha Young  Future Taifa Stars.
Akitangaza kikosi hicho jana, Kaim Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, kwa niaba ya Poulsen alisema makipa ni Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa na Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya).
Mabeki ni Aggrey Morris, Saidi Morad na Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Canavarro’ (Yanga) na Michael Pius (Ruvu Shooting).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni na Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas wa Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Athuman Idd na Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Amri Kiemba, Ramadhan Singano, Jonas Mkude na William Lucian (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting) na Salum Abubakar (Azam).
Kwa upande wa viungo washambuliaji ni Faridi Musa, Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa na Simon Msuva (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kutoka TP Mazembe ya DR Congo.
Kim amepanga kuitumia mechi hiyo ya kirafiki kupata nyota wa kuunda kikosi cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Heroes kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji.
Michuano hiyo mikongwe zaidi ambayo historia yake inaanzia mwaka 1926, wakati huo kama Gossage Cup kabla ya kuitwa Chalenji kuanzia mwaka 1973, itafanyika mjini Nairobi, Kenya, kuanzia Novemba 27.

Rage awabeba Kibadeni, Julio

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesema hawana mpango wa kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Abdallah ‘King’ Kibadeni.
Rage aliyasema hayo juzi kufuatia shinikizo kubwa la baadhi ya wanachama na viongozi kutaka kocha huyo na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ watimuliwe.
Hata hivyo, Rage alisema klabu hiyo haina sababu ya kumtimua Kibadeni kwani yu miongoni mwa makocha bora tena wa kupigiwa mfano nchini.
“Hakuna sababu ya msingi ya kumfukuza Kibadeni, amekosa nini? Kibadeni ni kati ya makocha bora nchini wenye mafanikio makubwa tangu uchezaji hadi ukocha,” alisema Rage na kuongeza:
“Kibadeni ndie mwenye rekodi ya kuwafunga Yanga mabao matatu katika ushindi wa 6-0; pia ndiye aliyeifikisha Simba fainali ya Kombe la CAF, mwaka 1993,” alisema.
Rage alisema anashangazwa na watu kutaka makocha hao watimuliwe bila sababu za msingi na kudai kuwa hakuna kocha atakayeondoka ndani ya klabu hiyo.
“Mpaka sasa Simba hatuna mpango wa kuwaondoa makocha wetu, watu wameamua kujisemea tu vitu wanavyovijua, lakini sisi bado tunaukubali mchango
wao na tutaendelea kuwa nao,” alisema Rage.

Kauli ya Rage imekuja huku Kamati ya Utendaji ikitaraji kukutana kesho kujadili mambo mbalimbali ya klabu hiyo, baada ya kushindwa kukutana juzi kama ilivyokuwa awali.

Fainali Kombe la Muungano 2014 kupigwa Zanzibar

MASHINDANO ya 19 ya Vijana ya Kombe la Muungano 2014 yanatarajiwa kuambatana na sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa mujibu wa Mratibu wa mashindano hayo, Daud Yassin, michuano hiyo itahusisha timu za mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa upande wa Bara na timu nne za Zanzibar. Mshindi wa Bara atacheza na mshindi wa Zanzibar, kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, ambako mchezo wa kwanza utachezwa Mufindi na fainali itapigwa Visiwani.
Yassin alisema tayari wameziandikia taasisi na kampuni mbalimbali kuomba udhamini huku wakiamini serikali nayo itawasaidia kufanikisha mashindano hayo yenye umaarufu mkubwa hapa nchini
Alifafanua kwamba wakiwa na Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Haji Salim, walifanikiwa kuonana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu,  aliyewaahidi kwamba serikali itaangalia namna ya kusaidia japo kidogo, ili kufanikisha mashindano ya mwakani, kwa kuzingatia kwamba mashindano hayo ya Muungano yataambatana na sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Kwa ujumla mashindano ya mwakani yatakuwa na msisimko mkubwa, huku timu shiriki, zikitakiwa kujiandaa vema na kuzingatia vigezo vya umri wa wachezaji usiozidi miaka 20 na kila timu inatakiwa kuwa na mwalimu angalau mwenye mafunzo ya awali ya ukocha,” alisisitiza mratibu huyo.
Yassin alisema wana matumaini makubwa kwamba wote walioombwa kudhamini michuano hiyo watakubali ili kuunga mkono jitihada za Kamati ya Kombe la Muungano, pamoja na ZFA, za kukuza na kuendeleza vipaji vya wachezaji vijana, sambamba na kuendelea kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kupitia michezo.
Aliongeza kwamba hata wale ambao hawajaombwa kudhamini, lakini wapo tayari kusaidia kufanikisha mashindano hayo ya mwakani wanakaribishwa.
Alisema kwa upande wa Bara hakutakuwa na timu mpya, bali zilizoshiriki mwaka huu, ndizo hizo hizo zitakazoshiriki mwakani, ikiwamo timu ya Mbeya City na vituo vya mashindano hayo kwa upande wa Bara vitakuwa Mufindi na Mbeya.
Alibainisha kwamba mambo yakienda sawa wanatarajia waamuzi wa kambi ya Twalipo ya Dar es Salaam watachezesha michuano hiyo.
mwanzo

Kwanini Hall amefukuzwa Azam FC?

NI ukweli unaoumiza kuwa mwanafunzi wa shule fulani aliyepata alama 34 za somo la Hisabati bado aliongoza darasani. Alipopelekwa shule nyingine, kiongozi wa somo hilo hilo alikuwa na alama 98. Haishangazi kwa nini Azam imeachana na Stewart Hall.
Azam inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini imegoma kukubali kuwa kwa uwekezaji wao mkubwa wanaoufanya hii ni nafasi halali kwao kuwepo. Hata kama wako pazuri, lakini kuna imani imejengeka Chamazi kuwa wanastahili kuwa mbali zaidi ya walipo sasa.
Hata kama wangekuwa wanaongoza ligi, lakini Azam ingejiuliza inaongoza Ligi kwa pointi ngapi? Katika huduma gani?Dhidi ya timu ambazo zimewekeza kwa kiasi gani? Zinacheza katika viwanja gani?
Kuwa na pointi sawa na Mbeya City hakuitendei haki Azam yenyewe, wala kupitwa pointi moja na Yanga hakuitendei haki Azam. Walipaswa kuwa juu ya hapo kwa vipimo walivyojiwekea wenyewe, lakini chini ya Stewart Hall haikuwa inaelekea huko.
Ashanti ilianza kukoleza safari ya Stewart
Wakati Yanga na Simba zikichota pointi sita na mabao tisa dhidi ya Ashanti, Azam iliambulia pointi moja tu dhidi ya timu hiyo na hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa Ashanti kupata pointi yake ya kwanza baada ya kuburuzwa tangu msimu uanze.

 


Wanasoka Wakenya wanaotajirika kupitia miguu yao

 


SOKA ni pesa. Ndivyo ilivyo duniani kote kwa sasa ambapo mchezo huo umegeuka na kuwa biashara kubwa kwa klabu na wachezaji husika.
Klabu zinaingiza fedha nyingi kwa mikataba minono ya udhamini na zawadi. Ndiyo maana nazo zimefungua neema kwa wachezaji na sasa zinawalipa mishahara minono na posho za uhakika, achilia mbali fedha za usajili inazowapatia.
Ndio maana wanasoka nao wamegeuka kuwa matajiri wakubwa, kwa Afrika wachezaji kama Samuel Eto’o na Michael Essien (wote Chelsea) na Yaya Toure wa Manchester City, ni miongoni mwa wanaotajwa kulipwa fedha nyingi.
Makala hii inakuletea orodha ya wanasoka 10 raia wa Kenya wanaolipwa vizuri katika klabu zao.

KILI STARS YAPANGWA NA ZAMBIA, BURUNDI CHALLENGE 2013

TANZANIA Bara maarufu kama Kilimanjaro Stars imepangwa katika Kundi B kwenye michuano ya CECAFA Challenge pamoja na Zambia, Burundi na Somalia.
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 27 mjini Nairobi, Kenya, wenyeji Harambee Stars wamepangwa na Ethiopia, Zanzibar na Sudan Kusini katika Kundi A.
Mabingwa watetezi, Uganda wamepangwa Kundi C pamoja na Rwanda, Sudan na Eritrea. Ratiba ya michuano hiyo inatarajiwa kutolewa wiki ijayo.

 

MAKUNDI CHALLENGE 2013:

KUNDI A- Kenya, Ethiopia, Zanzibar, South Sudan
KUNDI B- Tanzania, Zambia, Burundi and Somalia
KUNDI C- Uganda, Rwanda, Sudan and Eritrea.

 

ROSTAM AZIZ NDIYE BABA WA MATAJIRI WOTE TANZANIA, MENGI WA PILI AFRIKA NZIMA KATIKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI

TANZANIA imeongoza katika orodha ya tatu ya matajiri wapya wakubwa Afrika iliyotolewa na jarida la Forbes, mfanyabishara Rostam Aziz aliyeacha siasa kwa shinikizo la chama chake, CCM ili kubaki kwenye biashara pekee akitajwa kuwa tajiri zaidi nchini.
Rostam aliyejiuzulu Ubunge wa Igunga mwaka 2011, jarida la Forbes limesema ana utajiri wa thamani ya dola za Kimarekani Bilioni 1. 




                                                    KWA HABALI ZA    KIMATAIFA

Ronaldo v Zlatan mmoja lazima afe

MCHUJO wa kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil umeshika kasi kubwa na Ulaya kesho Ijumaa itakuwa na shughuli pevu kwa wapenda soka wakati itakaposhuhudia mafahari wawili, Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovich wakishuka uwanjani kuonyeshana ubabe.
Habari njema kwa mashabiki ni kwamba watashuhudia mastaa hao wakizitumikia timu zao Ureno na Sweden kwenye mechi hiyo yenye mvuto wa aina yake, lakini taarifa mbaya zinazidisha ugumu wa mechi hiyo kwamba ni lazima mmojawapo atakosekana safari ya Brazil mwakani.
Ronaldo na Zlatan wamekuwa gumzo duniani kwa sasa kufuatia mchezo huo wa mchujo ambao wa kwanza utafanyika Ureno kabla ya mechi yao ya marudiano itakayofanyika nchini Sweden wiki ijayo.
Mechi hiyo imevuta hisia za wengi tofauti na nyingine zinazohusu kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia kutokana na mastaa hao wawili kuwa na idadi kubwa ya mashabiki ambao kila upande unavuta kwake.
Mechi nyingine za mchujo wa upande wa Ulaya kesho Ijumaa, Ufaransa itamenyana na Ukraine, Ugiriki itakipiga na Romania na Iceland itapepetana na Croatia ikiwa ni mechi za raundi ya kwanza.



Beckham, Zidane kung’ara kwenye sinema
SUPASTAA David Beckham anatarajia kung’ara na wakali wengine wa Manchester United, Ryan Giggs, Paul Scholes, Nicky Butt na ndugu wawili wa familia ya Neville kwenye filamu iliyoandaliwa na Universal Pictures itakayoanza kuonekana kwenye kumbi za sinema mwezi ujao.
Wachezaji hao walioibukia kwenye kikosi cha Manchester United na kubachikwa jina la ‘The Class of ‘92’, walipata mafanikio makubwa ikiwamo kunyakua mataji matatu katika msimu mmoja mwaka 1999.
Lakini, ndani ya filamu hiyo kutakuwa na majina mengine makubwa kwenye soka; Eric Cantona na Zinedine Zidane, ambao wamezidi kuipa utamu zaidi sinema hiyo.
“Kipindi changu cha maisha na wachezaji hawa pale Manchester United kilikuwa cha kipekee,” alisema Beckham.
“Tulikuwa kutoka sehemu zenye utamaduni tofauti, lakini tulikuwa pamoja na kuwa kama familia moja na sote tulitaka mafanikio. Mwisho wa yote tulifikia mafanikio yetu na kutimiza ndoto. Kweli  nimependa kutengeza filamu hii kwa sababu imetuleta pamoja tena.”
Giggs, ndiye mchezaji pekee kutoka kwenye kundi hilo anayeendelea kucheza hadi sasa.
Wakati huohuo, Beckham ameripotiwa kushitushwa na kusikia taarifa za kifo cha bibi yake mzaa mama, Peggy West. Bibi wa staa huyo wa zamani wa England alifariki Dunia Ijumaa iliyopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kupooza.



ASNTE KWA USHILIANO WAKO WAKUSOA HABALI ZA MICHEZO
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top