Jumapili, 10 Novemba 2013



Juma Kaseja Sasa Anamilikiwa Na Klabu Ya Yanga Kwa Mkataba Wa Sh Milioni 40




Mlinda mlango bora Tanzania Juma Kaseja amesaini Mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga kwa dau la Sh Milioni 40.Kaseja ametia wino kwenye mkataba huo akiwa na vigogo wa Usajili wa Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb na Seif Ahmed Magari’ mbele ya Meneja wake, Abdulfatah Salim Saleh Ilala jijini Dar es Salaam.

Kaseja atakuwa klabu moja na makipa wawili aliowahi kufanya nao kazi Simba SC Ally Mustafa Barthez na Deo Munishi Dida.


Hii inakuwa mara ya pili Kaseja kusajiliwa Yanga, baada ya awali kusajiliwa miaka mitatu iliyopita akitokea Simba SC ambako baada ya msimu mmoja wa Mkataba wake kuisha alirejea Msimbazi. Alitemwa na simba wakati huo kwa sababu ya kiwango kushuka.

 Yanga SC itanufaika na uzoefu wake katika game za kimataifa na inataka inufaike naye katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2014.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top