CECAFA CHALLENGE CUP DRAW
This is to inform you that the draw for the CECAFA Challenge cup
2013 in Kenya was held today in Nairobi. And the drawing of lots are as
follows:-
GROUP A- Kenya, Ethiopia, Zanzibar, South Sudan
GROUP B- Tanzania, Zambia, Burundi and Somalia
GROUP C- Uganda, Rwanda, Sudan and Eritrea.
The fixtures will be released next week.
RONALDO VS ZLATAN: JOHAN CRUYFF ATAJA ANAYETAKA AMUONE AKIFUZU KWENDA KOMBE LA DUNIA
Gwiji wa soka wa Uholanzi Johan Cruyff angependa kuona Cristiano Ronaldo akienda kucheza kombe la dunia 2014 mbele ya Zlatan Ibrahimovic.Nyota huyo wa zamani wa Barcelona amesema kwamba ni jambo baya kuona aidha Ronaldo au Ibrahimovic wakikosa nafasi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa ya dunia, lakini angependa zaidi kumuona staa wa Ureno Cristiano Ronaldo akifuzu na timu yake mbele ya Sweden ya akina Ibrahimovic.
"Ni jambo baya kwa kombe la dunia kwamba mmoja kati ya washambuliaji bora duniani hatoweza kucheza michuano hiyo. Ni ni jambo la kuhuzunisha," Cruyff aliiambia Algemeen Dagblad.
"Sina yoyote ninayempendelea kati ya hawa wawili, lakini nikitakiwa kuchagua mmoja kati yao yupi ningependa kumuona akiingia World Cup na timu yake, basi ningependa kumuona Ronaldo akifuzu."


0 maoni:
Chapisha Maoni