Jumatano, 16 Oktoba 2013

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Nchini (Necta), Dk Joyce Ndalichako, ameanza likizo ya mwaka mmoja kwa kile kilichoelezwa kuwa anafanya utafiti juu ya uendeshaji wa mitihani nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam Dk Charles Msonde ambaye  anakaimu nafasi hiyo amesema Dk Ndalichako amechukua likizo ya mwaka mmoja ambayo itamalizika september mwaka kesho
Katika kipindi cha mwaka mmoja Ndalichako atakuwa anafanya utafiti unaohusu uendeshaji wa mitihani nchini na kuangalia suala la matumizi ya alama za maendeleo za mwanafunzi (continuous assessment (CA)
Hivi karibuni Dr Ndalichako alieleza masuala mbali mbali ambayo nitishio kwa baraza la mitihani  kuwa ni pamoja na mtazamo wa watu ambao kwa kiasi kikubwa wanakataa ukweli na mabadiriko

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top