Mwenyekiti wa CHADEMA Arusha, Samson Mwigamba asimamishwa uongozi, baada ya kukiri kusema uongo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa
Arusha, Ndugu Samson Mwigamba amesimamishwa nafasi ya uongozi hiyo mara moja
kuanzia leo na Baraza la Uongozi la Kanda ya Kaskazini, huku taratibu zingine
za kinidhamu zikiendelea kwa kufuata katiba, kanuni, maadili, miongozo na
taratibu za chama.
Kikao hicho kimechukua hatua
hizo mara moja baada ya Ndugu Mwigamba kukiri kwa maandishi kuwa ameandika kwa
kutumia jina bandia na kutuma kwenye mitandao ya kijamii, kutoa tuhuma za uongo
na kupotosha umma dhidi ya chama na viongozi, kinyume na katiba, kanuni,
maadili, miongozo na taratibu za chama.
Hatua hiyo ya kukiri na
kusimamishwa uongozi, ilifuatia baada ya Ndugu Mwigamba kutuhumiwa kusambaza
katika mitandao tuhuma za uongo, upotoshaji na uchonganishi, ambapo kikao
kilimwagiza kusalimisha kompyuta yake ili wataalam wa masuala ya IT wa CHADEMA,
Kanda ya Kaskazini, waweze kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Wataalam hao wa masuala ya
IT, wakitumia ushahidi uliokuwa katika bandiko hilo, hasa jina la kiongozi
huyo, walibaini pasi na shaka kuwa andiko lililosambazwa kwenye mitandao ya
kijamii, kwa kutumia jina bandia liliandikwa na kuhifadhiwa kwenye kompyuta ya
Mwigamba kisha kupostiwa leo.
Ndugu Mwigamba ametuhumiwa
kusambaza andiko hilo akiwa katikati ya kikao, baada ya amemaliza kuwasilisha
taarifa ya hali ya chama katika mkoa wake wa Arusha, ambapo alikisifia chama na
uongozi wa taifa kwa kutekeleza maagizo ya vikao vya chama na kubuni mipango na
mikakati mbalimbali ya kukiendesha chama ili kuiondoa CCM madarakani.
Kikao hicho cha Baraza la Uongozi, chini ya uenyekiti wa Mh. Israel Natse, Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini (Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Arusha), kiliazimia kwa kauli moja kumsimamisha Mwigamba, huku taratibu zingine za kushughulikia masuala ya kinidhamu zikifuata.
Kikao hicho cha Baraza la Uongozi, chini ya uenyekiti wa Mh. Israel Natse, Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini (Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Arusha), kiliazimia kwa kauli moja kumsimamisha Mwigamba, huku taratibu zingine za kushughulikia masuala ya kinidhamu zikifuata.
0 maoni:
Chapisha Maoni