
Rapper Ney Wa
Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea Jana wakati wana
shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa kwenye radio stations '
Salam Zao'.
Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli
nilitupwa sero jana baada ya raia wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi
yangu kwasababu kulikuwa na waigizaji waliokuwa na sare za polisi. Watu
hao sijuani nao na walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia
sare za polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea
nikapelekwa polisi.
Mitego ameendela kusema kuwa baada ya kuka sero kwa dakika kama 15 mkuu wa
kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya kutoa
maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuonekana uraiani.
Ney aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki
ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania.
0 maoni:
Chapisha Maoni