Jumapili, 13 Oktoba 2013



Kocha: Juma Kaseja anawafunika wote


KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja ametamka kuwa, hajaona kipa mzuri Tanzania kama, Juma Kaseja na hana mpinzani kwa sasa kwa sababu ana kila kitu.
Katika hatua nyingine, Mayanja pia alimtaka Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen aache kukariri wachezaji wa Simba, Yanga na Azam FC na kuwaita Stars.

Mayanja ambaye ni raia wa Uganda alisema: “Kwa Tanzania sijaona kipa kama Kaseja na wanaposema ameshuka kiwango nawashangaa sana. Wachezaji wa ndani viwango vyao vinafanana, wa Mbeya City, Kagera Sugar, Simba na Yanga wote sawa. Hao wa Simba na Yanga mnawaona

wazuri wanalindwa na uzoefu tu labda Chuji tu (Athuman Idd) ambaye mimi nasema hastahili kucheza Tanzania, kiwango chake ni Ulaya tu.”

“Chuji alitakiwa kucheza ligi kubwa za Afrika au Ulaya si Yanga inayofanyia mazoezi mchangani.
Akimzungumzia Poulsen, Mayanja alisema: “Poulsen anakariri na kudhani wachezaji wazuri wapo timu tatu za Simba, Yanga na Azam tu jambo ambalo anakosea. Ukiangalia timu za mikoani zina wachezaji wazuri hawa wa Simba, Yanga na Azam wanawazidi wale kwa sababu ya uzoefu tu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top