Msanii
wa muziki wa kizazi kipya nchini Madee ameweka wazi kuwa nyimbo yake ya
'Nani kamwaga pombe yangu' imemuingizia mtonyo zaidi ya milioni 140.
Akizungumza
katika moja ya mahojiano ndani ya radio ya Clouds FM Madee aliweka wazi
kuwa hiyo ndiyo nyimbo yake ya kipekee iliyomuingizia hela kwa muda
mfupi hali iliyopelekea kubadili aina ya muziki kuacha muziki wa Hip Hop
na kuamini kuwa staili anayoifanya sasa ndiyo ipo kwenye biashara.
Msanii
huyo ameweza kukusanya mtonyo huo katika shoo mbalimbali ambapo aliweka
mchanganuo wa shoo zake kuwa aliweza kupata shoo 8 za fiesta, pia
aliweza kuingia mkataba na kampuni za simu ambapo aliweza kukusanya
zaidi ya milioni 80 pamoja na kampuni ya Coca Cola.
Jumapili, 13 Oktoba 2013
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni