Jumamosi, 12 Oktoba 2013

HABARI FUPI


                                                 habari fupi
*Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bw Pereila Sirima kesho anatarajia kufanya ziara ya siku mbili mkoani Singida
Katibu wa jumuiya ya wazazi mkoani singida Bw Julius Mbwiga amesema akiwa mkoani Singida atatembelea wilaya za Singida vijijini, Singida mjini pamoja na mkalama na kukagua shughuli za maendeleo na kuhimiza uhai wa shuhuli za jumiya ya wazazi

*Naibu waziri wa katiba na Sheria, Angellah Kairuki, amesema kukosekana kwa walimu wa lugha ya alama, kumesababisha wanafunzi 39 kati ya 40 wenye ulemavu wa kutosikia waliomaliza elimu ya sekondari mwaka jana kupata daraja sifuri
Akizungumza mjini Dar es Salaam Kairuki amesema changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu huo kwa elimu ni kutokuwa na fursa sawa ya kutumia lugha wanayomudu

*Rais Armando Guebuza wa Msumbiji amesema watu wanaofanya uhalifu wa kikatili wanatakiwa kuhukumiwa na mahakama za ndani na sio kuwapeleka kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ambayo utendaji wake ni wa aina nyingine ya kutokuwa na haki.
Akiongea mjini Kampala, Rais Guebuza amesema si haki kwa mahakama hiyo kuwachukulia hatua waafrika wakati wapo wengine wanaofanya uhalifu mkubwa kuliko ule unaofanywa na waafrika lakini hawafikishwi kwenye mahakama hiyo
*Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha mpango uliopendekezwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Ban Ki Moon kuhusu kuondoa silaha za kemikali nchini Syria kwa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na shirika ka kupiga marufuku silaha za kemikali
Mabalozi wa Uingereza na Russia kwenye Umoja wa Mataifa wamesema wajumbe wote 15 wa baraza la usalama wamepitisha mpango huo unaoendana na azimio namba 2118 la baraza la usalama lililopitishwa mwishoni mwa mwezi uliopita,
Tayari kazi ya kuteketeza baadhi ya viwanda vya silaha za kemikali na baadhi ya kemikali zimeanza kutekelezwa na serikali ya Syria chini ya usimamizi wa shirika la kupiga marufuku silaha za kemikali

                                          asante
Chapisho Jipya
Previous
This is the last post.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: HABARI FUPI Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top