Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ana wasiwasi kuhusu matokeo ya timu yake na anasema wachezaji wake wanafaa kuimarika baada ya kushindwa 2-1 na kilabu ya Swansea.
Mauricio Pochettino,wakati huohuo amekataa kulaumu mtu baada ya timu yake ya Tottenham Hotspur inayopigania kuchukua ligi msimu huu kupoteza kwa West Ham 1-0.
Na mkufunzi wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema kuwa hafikirii kushinda taji la ligi ya Uingereza baada ya timu yake kucharazwa 3-0 na Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Hiyo inamaanisha kwamba Leicester itasalia kileleni mwa ligi huku ikiwa kumesalia mechi 10 pekee.
Leicester ina pointi 57, na hivyobasi wameongeza uongozi wao katika jedwali la ligi hiyo baada ya sare ya 2-2 dhidi ya West Bromwich.
Ushindi huo wa Swansea unamaanisha kwamba Arsenal imepoteza mara tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010.
0 maoni:
Chapisha Maoni