Jumanne, 22 Machi 2016

WANANCHI NA VIONGOZI MKOANI SINGIDA WAMETAKIWA KUSHILIKI VEMA KATIKA ULINZI WA WANYAMA POLI.


Wakili wa serikali mkuu mfawidhi mkoani Singida,Zakaria Elisaria Ndasikowe,amewataka wakazi mkoani Singida kutambua kwamba wana wajibu wa kushauriki na kulinda wanyamapori wakiwemo tembo dhidi ya majangili,ili rasilimali hiyo iendelee kunufaisha kizazi cha sasa na kile kijacho.
Bw Zakaria amesema hayo wakati akizungumzia juu ya mafanikio waliyoyapata ya kukusanya ushahidi uliofanikisha  majangili 13 kufungwa jela

Aidha amesema  ofisi yake wamejipanga kukusanya ushahidi dhidi ya watuhumiwa wa ujangili,ili waweze kupewa adhabu stahiki pindi wanapofikishwa mahakamani.

Amesema wanaamini adhabu zinazotolewa na mahakama ya mkoa huu,zitakuwa fundisho kubwa kwao na vile vile zitawaogopesha watu wachache wanaotarajia kujihusisha na uwindaji haramu, unaotishia kutoweka kwa wanyamapori.


Wakili huyo mkuu,ametumia nafasi hiyo kuwataka watanzania hao wachache wanaojitafutia utajiri kupitia uwindaji haramu,kuacha mara moja uwindaji huo haramu,kwa madai utawasababishia matatizo makubwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: WANANCHI NA VIONGOZI MKOANI SINGIDA WAMETAKIWA KUSHILIKI VEMA KATIKA ULINZI WA WANYAMA POLI. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top