Jumatano, 9 Machi 2016

MATOKEO YOTE YA VPL MECHI ZA MARCH 9, 2016 NA MSIMAMO WA VPL

Ligi kuu Tanzania bara imeendelea leo kwa michezo minne kuchezwa kwenye viwanja tofauti vya miji ya Tanzania bara.
Mwadui FC ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Mwadui Complex, Shinyanga imebanwa mbavu na Majimaji ya Songea, Ruvuma kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana.
Kagera Sugar ambayo kwa sasa inanolewa na kocha Adolf Rishard imeilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 timu ya wajelajela Tanzania Prisons ya mbeya kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Coastal Union imeweza kujinasua kutoka mkiani mwa ligi baada ya kuinyuka Mgambo JKT kwa bao 1-0 mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wao uliopita kwenye dimba la Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, JKT Ruvu imevuna ushindi mwingine leo kwenye uwanja huo kwa kuichapa Toto Africans kwa bao 2-0 na kuendelea kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi
Matokeo yote ya mechi za VPL zilizochezwa leo yapo kama ifuatavyo
Mwadui FC 0-0 Majimaji FC
Tanzania Prisons 1-1 Kagera Sugar
Coastal Union 1-0 Mgambo JKT
JKT Ruvu 2-0 Toto Africans
Msimamo 1

Msimamo
Msimamo 1
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: MATOKEO YOTE YA VPL MECHI ZA MARCH 9, 2016 NA MSIMAMO WA VPL Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top