SIMBA SC imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shukrani kwao, washambuliaji Ibrahim Hajib na Daniel Lyanga aliyetokea benchi kipindi cha pili na waliofunga mabao hayo, yanayoifanya Simba sasa ifikishe pointi 48, baada ya kucheza mechi 21.
Mabingwa watetezi, Yanga na Azam FC wenye pointi 47 za mechi 20 kila mmoja, wanafuatia katika nafasi ya pili nay a tatu.
Awadh Juma na Daniel Lyanga kulia wakishangilia na Ibrahim Hajib aliyepiga magoti baada ya kufunga bao la pili dakika ya 90. Kushoto ni kipa wa Mbeya City, Hannington Kalyesebula akiwa ameketi mkao wa "Nifanyeje" |
Hajib akafunga la pili dakika ya 90 baada ya kuwatoka mabeki wa Mbeya City na kupiga shuti la mbali kama krosi, lililotinga nyavuni moja kwa moja.
Simba ingeweza kushinda mabao zaidi kwenye mchezo huo kama ingetumia vizuri nafasi ilizotengeneza tangu kipindi cha kwanza.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Emery Nimubona/Hassan Kessy dk68, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Juuko Murshid, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Hamisi Kiiza/Awadh Juma dk59, Ibrahim Hajib na Brian Majwega/Daniel Lyanga dk46.
Mbeya City: Hannington Kalyesebula, Hassan Mwasapili, Abubakar Shaaban, Tumba Swedi, Haruna Shamte, Kenny Ally, Raphael Alpha, Haruna Moshi/Themi Felix dk68, Geofrey Mlawa, Joseph Mahundi na Ditrim Nchimbi/Ramachani Chombo ‘Redondo’ dk83.
0 maoni:
Chapisha Maoni