Jumapili, 20 Machi 2016

BPL: ARSENAL WAIBUKA, MABINGWA CHELSEA WACHOMOA KWA TUTA MWISHONI, LEICESTER WACHANJA KUELEKEA TAJI!


>>JUMAPILI MTANANGE ETIHAD DABI YA MANCHESTER, CITY V MAN UNITED!
LIGI KUU ENGLAND
Matokeo
LIGI KUU ENGLAND
**Saa za Bongo
Jumamosi Machi 19
Everton 0 Arsenal 2          
Chelsea 2 West Ham 2               
Crystal Palace 0 Leicester 1                  
Watford 1 Stoke 2            
West Brom 0 Norwich 1              
2030 Swansea v Aston Villa        
+++++++++++++++++++
BPL-LEICESTER-USHINDIKwenye Mechi za BPL, Ligi Kuu England, zilizochezwa hii Leo, Mabingwa Watetezi Chelsea, wakiwa kwao Stamford Bridge, walisawazisha kwa Bao la BPL-MAR19Dakika ya 88 la Penati ya Cesc Fabregas lakini habari ya ‘Mujini’ ni Vinara Leicester City kuendelea kuzoa Pointi na kuchanja mbuga kileleni.
Leicester, wakicheza Ugenini huko Selhurst Park waliifunga Crystal Palace 1-0 kwa Bao la Riyad Mahrez la Dakika ya 34 ambalo limefungua pengo la Pointi 8 na Timu ya Pili Tottenham.
Arsenal, ambao mapema walicheza Ugenini huko Goodison Park, waliifunga Everton 2-0 kwa Bao za Danny Welbeck na Tineja Alex Iwobi na kufuta machungu ya Wiki mbaya ambayo iliwakumba kwa kutupwa nje ya FA CUP na UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Huko Stamford Bridge, Mabingwa Watetezi Chelsea mara mbili walitoka nyuma kwa West Ham waliofunga Bao zao kupitia Lanzini na andy Carroll na mara mbili Fabregas kuwakomboa kwa Bao za Frikiki na Penati.
Kesho Jumapili ni Siku ya Dabi mbili moja ikiwa ya huko Manchester ndani ya Etihad kati ya City na Man united.
VIKOSI:
Leicester City: Schmeichel; Simpson, Huth, Morgan, Fuchs; Mahrez, Kante, Drinkwater, Albrighton; Okazaki, Vardy
Akiba: Schwarzer, Wasilewski, Amartey, Inler, Gray, Schlupp, Ulloa.
Newcastle United: Elliott; Janmaat, Taylor, Lascelles, Colback; Sissoko, Anita, Shelvey, Perez; Wijnaldum; Mitrovic
Akiba: Darlow, Sterry, Saivet, Townsend, De Jong, Riviere, Doumbia
REFA: Craig Pawson
LIGI KUU ENGLAND
**Saa za Bongo
Jumapili Machi 20
1630 Newcastle v Sunderland               
1630 Southampton v Liverpool             
1900 Man City v Man United                
1900 Tottenham v Bournemouth   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: BPL: ARSENAL WAIBUKA, MABINGWA CHELSEA WACHOMOA KWA TUTA MWISHONI, LEICESTER WACHANJA KUELEKEA TAJI! Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top