Jumatano, 24 Februari 2016

Usisahu kuwa Yanga imecheza leo dhidi ya JKT Mlale FA Cup, matokeo haya

Jumatano ya February 24 klabu ya Dar Es Salaam Young African ilikuwa mwenyeji wa klabu ya JKT Mlale katika mchezo wao wa hatua ya 16 bora yaa Kombe la FA ambalo linafahamika kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Yanga walishuka uwanja waTaifa wakiwa wamebadili kikosi chao tofauti na kilivyozoeleka.
Kikosi cha Yanga ambacho kilisaidia kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya JKT Mlale, kiliamua kuwaanzisha wachezaji kama Matheo Anthony na Geofrey Mwashiuya naSaid Juma, kwa kile ambacho kinaaminika ni kuwapumzisha wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mechi ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya klabu ya Cercle de Joachimya Mauritius.
Yanga walianza kwa kuruhusu goli, baada ya Shabani Mgandila kutumia vyema makosa ya safu ya ulinzi na kupatia goli la kwanza dakika ya 22, licha ya kuwa Yanga walikuwa wanajiamini na kucheza kwa dharau, walifanikiwa kusawazisha goli dakika ya 38 kupitia kwa Paul Nonga na dakika ya 58 Thabani Kamusoko akapachika goli la pili na la mwisho kwa Yanga baada ya kutumia vyema pasi ya Geofrey Mwashiuya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Usisahu kuwa Yanga imecheza leo dhidi ya JKT Mlale FA Cup, matokeo haya Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top