Jumanne, 23 Februari 2016

Obama atoa mpango wa kufunga jela ya Guantanamo

Rais wa Marekani Barack Obama amewasilisha mpango wa kufungwa kwa jela ya Guantanamo Bay, moja ya malengo yake ambayo bado alikuwa hajatimiza.
Habari hizo zimetangazwa na ikulu ya White House.
Wizara ya ulinzi ya Marekani imependekeza wafungwa 91 ambao bado wanazuiliwa katika gereza hilo warejeshwe nchi zao asili au wahamishiwe magereza ya jeshi la Marekani au magereza ya kiraia.
Lakini Bunge la Congress limekuwa likipinga wazo hilo na linatarajiwa kupinga mpango huo wa Rais Obama.
Gereza hilo hugharimu Marekani $445m (£316m) kila mwaka.
Image copyrightAP
Maafisa wakuu wa utawala wake waliambia wanahabari Jumanne kwamba kufungwa kwa jela hiyo ni hitaji la usalama wa kitaifa.
"Kutekelezwa kwa mpango huu kutaimarisha usalama wa taifa kwa kuwanyima magaidi ishara muhimu ambayo wamekuwa wakitumia katika propaganda, kuimarisha uhusiano na marafiki wakuu na washirika katika kukabiliana na ugaidi, na kupunguza gharama,” afisa wa vyombo vya habari wa Pentagon Peter Cook amesema kupitia taarifa.
Watu 780 walizuiliwa Guantano tangu 2002, lakini kwa sasa ni 105 pekee waliosalia gerezani. Hamsini kati ya hao wameidhinishwa kuachiliwa huru.
Jela hilo ilijengwa na Marekani baada ya amshambulio ya tarehe 11 Septemba mwaka 2001 na hutumiwa na Washington kuwazuilia „wapiganaji maadui”.
Rais Barack Obama amesema anataka kufunga gereza hilo kabla ya kuondoka madarakani mapema 2017.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 maoni:

Chapisha Maoni

Item Reviewed: Obama atoa mpango wa kufunga jela ya Guantanamo Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top