Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE baada ya kupoteza mchezo wa watani kwa kufungwa 2-0 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mkude amesema kwamba wamesikitishwa mno na matokeo hayo, lakini wanapswa kusimama imara na kusonga mbele.
Jonas Mkude ameomba mshikamano Simba SC |
“Kama ilivyo kaulimbiu yetu Simba, Nguvu Moja, sasa tutawekeza nguvu zetu kwenye michezo inayofuata na ni matumaini yetu bado wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba tutakuwa pamoja katika kuendelea kuhakikisha kuwa ubingwa msimu huu unakuja Msimbazi,” amesema.
Simba SC ilipokonywa usukani wa Ligi Kuu baada ya kuchapwa 2-0 watani wao, Yanga mabao ya Mzimbabwe Donald Ngoma kipindi cha kwanza na Mrundi Amissi Tambwe kipindi cha pili.
Matokeo yaliifanya Yanga ifikishe pointi 46 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda kileleni, wakati Simba SC iliyocheza mechi 20, inaporomoka hadi nafasi ya tatu ikibaki na pointi zake 45, sawa na Azam FC nayopanda nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao (GD).
0 maoni:
Chapisha Maoni